Wednesday, February 19, 2014

UGANDA WATUNGA SHERIA KALI KWA WANAOVAA 'MINI SKIRT'


Maandamano ya kupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kampala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

BOKO HARAM BADO NI HATARI NIGERIA

Wapiganaji wa Boko Haram
Taarifa kutoka nchini Nigeria, zinasema kuwa kumekuwa na mashambulizi mabaya sana dhidi ya wakazi wa mji wa mpakani wa Bama, siku moja baada ya msemaji wa Rais kusema kuwa jeshi linashinda vita dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram.
Seneta wa jimbo la Borno, Ahmed Zanna ameambia BBC kuwa mashambulizi hayo yaliyotokea Jumatano asubuhi yalidumu kwa masaa 5
Siku ya Jumanne, msemaji wa jeshi Doyin Okupe, alisema kuwa jeshi limeweza kudhibiti hali.
Zaidi ya watu 254 wameuawa mwaka huu pekee na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Maelfu wameuawa tangu Boko Haram kuanza vita dhidi ya serikali mwaka 2009.
Taarifa ya bwana Okupe, ilitofautiana na matamshi ya gavana wa jimbo la Borno ambalo ni kitovu cha Boko Haram.
Gavana Kashim Shettima, ametoa wito wa kutaka wanajeshi zaidi na ambao wamejihami vilivyo kupelekwa katika jimbo hilo, kuliko vikosi vya usalama vilivyoko katika jimbo hilo.
Taarifa kuhusu mashambulizi ya leo bado hazitajitokeza lakini wakazi wa eneo hilo wamewasiliana na idhaa ya BBC Hausa kuhusu mashambulizi ya leo. Mji huo hata hivyo umewahi kushambuliwa katika siku za nyuma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo BBC

TAHADHARI YA MVUA KUBWA FEB 19-21/2014

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706

FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti:  www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 18 Februari, 2014

TAARIFA KWA UMMA: VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA.
Taarifa Na. 201402-03
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 8:30 Mchana

Daraja la Taarifa:- Tahadhari
Kuanzia: Tarehe 19  Februari, 2014 

Mpaka: Tarehe 21 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa ni vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kwa siku.

Kiwango cha uhakika:- Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni Kanda ya kati (mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe) na maeneo ya kusini  (Mikoa ya Ruvuma na Morogoro).

Maelezo:-
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo 
wa hewa katika rasi ya Msumbiji. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta 
upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo:-
Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo 
hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.

Maelezo ya Ziada:-
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa 
mrejeo kila itakapobidi.

Imetolewa na 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Monica Mutoni
Public Relation Office
Tanzania Meteorological Agency

VITA VYAZUKA TENA MALAKAL, SUDAN KUSINI

Haya ni mapigano ya kwanza tangu kutia saini mkataba wa kusitisha vita
Mapigano yanaripotiwa kuzuka Sudan Kusini kwa mara ya kwanza tangu serikali na waasi kutia saini makubaliano ya kusitisha vita mwezi Januari.
Waasi wanaomtii makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, wameshambulia mji wa Malakal, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile linalozalisha mafuta kwa wingi.
Majeshi ya serikali, yamepambana vikali na waasi hao katika maeneo tofauti ya mji huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Juba, (Toby Lanzer), amezitaka pande zote kwenye mzozo huo, kulinda raia.
Makabiliano hayo bila shaka yanazua wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika visima vya mafuta Kaskazini mwa nchi. Mafuta ya Sudan Kusini ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo BBC Swahili

CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE...!!!

Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi ndani ya siku tatu, vinginevyo suala hilo litafikishwa jumuiya za kimataifa.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo Chadema wanaitafsiri kama kielelezo cha kuvuruga amani ndani ya nchi.
Kwa majibu CCM kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamwe hawatafanya hivyo.
"Kauli aliyoitoa Rais Kikwete ni ndogo na kutokana na vitendo vinavyofanywa na viongozi na wanachama wa Chadema kuvuruga amani nchini," alisema na kuongeza kuwa dawa ya moto ni moto.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa Chadema, Benson Kigaila alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kufuta alichokizungumza ndani ya siku tatu kuanzia jana, vinginevyo watalifikisha suala hilo mbele ya jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya malalamiko yao.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu, na alihoji kwanini awatake WanaCCM kujibu mapigo dhidi ya wapinzani badala ya kuacha hatua za kisheria zikafuatwa kwa kutumia vyombo husika ambavyo ni polisi na majeshi na mahakama. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo:Mwananchi

MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 19, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MATOKEO YA MANCHESTER CITY vs BARELONA

Screen Shot 2014-02-19 at 7.09.55 AM 
Kwenye zile game za UEFA ambazo zitaingia kwenye rekodi ya kutazamwa na mamilioni mwaka 2014 na hii imo ambapo Manchester City wamefungwa goli mbili zote kwenye kipindi cha pili.
Screen Shot 2014-02-19 at 7.11.49 AM 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WACHEZAJI WATATU KUFUATA NYAYO ZA AKINA MBWANA SAMATTA

Wadau wengi wa michezo wanakua wakiwaangalia sana wachezaji waliotoka Bongo kwenda nje ya nchi kucheza soka la kulipwa na miongoni mwao ni Mbwana Samatta ambaye kwa mshahara wake peke yake umezua gumzo mtaani,
Sasa taarifa kutoka TFF ambayo ame-amplify Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura unaambiwa Wachezaji watatu kutoka Tanzania ambao ni wachezaji wa mpira wa miguu tayari wameombewa hati ya uhamisho wa Kimataifa[ITC] ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.
Miongoni mwao ni mchezaji Khamis Mroki Jamal ambaye timu yake ilikua Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam yeye ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.
Wengine ni Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo hao wote wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.
Kwa sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania TFF itatoa ITC hizo na jamaa kwenda kujiunga na timu hizo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TCIB: WAGOMBEA UCHAGUZI WAPIMWE AFYA


kibamba_9c593.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kubadilisha mfumo wa uendeshaji Uchaguzi Mkuu ikiwamo kuweka kipengele kitakachowalazimisha wagombea wa nafasi za uongozi kupima afya zao ili kuepuka kuchaguliwa viongozi wenye maradhi yatakayowafanya washindwe kumudu majukumu yao ya kazi.
Pia kimeitaka NEC kuweka zuio la kufanyika kwa uchaguzi na kutoza faini kali kwa mgombea anapotangaza kujitoa katika hatua za mwisho kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba wakati akitoa tathimini ya uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika Kata 27 na funzo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ule wa Ubunge katika Jimbo la Kalenga mwezi ujao.
Alisema, Novemba 2012 kulifanyika uchaguzi kujaza nafasi 29 za udiwani wakati Juni 2013 kulifanyika tena uchaguzi katika kata 22 na mwezi huu umefanyika uchaguzi katika kata 27, huku baadhi ya kata zikiwa tayari zimekwisharudia chaguzi zaidi ya mara moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...