Thursday, April 25, 2013

WIMBI LA MAKAHABA LAZIDI KUONGEZEKA JIJINI DAR, COCO BEACH YAGEUZWA 'GUEST BUBU' NYAKATI ZA USIKU...!!

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai  alivyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha. Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).
BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.
ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.
MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.
MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungw

a alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.
INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea.
Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.

LULU AINGIA MZIGONI RASMI NA KUFYATUA FILAMU YAKE........!!!

HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.

Baadhi ya picha hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina lake halijapatikana.
 

Mara baada ya kutupia picha hizo mtandaoni, watu mbalimbali walimtumia ujumbe kumsifia kwa kumwambia kuwa ana kipaji cha kazi hiyo.

Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo naye alichangia mada hiyo na kumsifu Lulu kwa uwezo wake wa kuigiza.
Lulu amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kupata msala wa kumuua bila ya kukusudia staa mwingine wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka jana, hivi sasa yuko nje kwa dhamana.

Diamond ashindwa kutamba tunzo za Kili 2013, hawa ndio waliotajwa


Msanii bora wa hiphop
Fid Q, 
Joh Makini, 
Kala Jeremiah, 
Profesa J, 
Stamina

Wimbo bora wa Mwaka: 
Dear God Kala Jeremiah,
Leka Dutigite

LULU AINGIA KATIKA SKENDO HII MPYA..........!!!

 
 
NAHISI HII NDO ITAKUA SKENDO YA KWANZA INAYOMHUSU LULU BAADA YA KUTOKA SELO. LEO KATIKA PITA PITA YANGU NIMEPITA KATIKA WEBSITE YA SINTAH NA KUKUTANA NA POST YENYE KICHWA CHA HABARI "THE RETURN OF HOTLULU" KAMA ILIVYOANDIKWA NA SINTAH MWENYEWE. SO KA ROHO KAKANITUMA NISOME COMMENTS. KI UKWELI COMMENTS NYINGI ZILIKUA NI ZA KUMPONDA SINTAH BUT NIKAKUTANA NA COMMENT MOJA ILIYOTOLEWA NA MTU AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LITAJWE IKIWA NA MAONI HAYA
" Sintah for sure mwambie huyu mtoto akae mbali na BONITA atamuharibia dakika moja. Jana nilipita pale nje maeneo ya deMage hotel kwenye duka uchwara la BONITA, nkaona gr la Lulu na kuna gr lingine la mvulana fulani mtoto wa daaud kanyau aitwae POnchi. Nimejua tu nn kinaendelea mule ndan,.baada ya dk kadhaa Lulu alitkoka ndn ya duk Nawakaingia kwny gari la ponchi wakaongea humo then ponchi akaondoka. Plz, plz plz plz naomba awe makini ikibd akae mbali sana n BONITA. BONITA ni kuwadi mkubwa sana. Ilimradi yy apate pesa hajali mtoto wala mkubwa. Ntafatulia hii inshu nikupe zaid yalio jiri. I love lulu kipindi hiki awe makini"

NAKAAYA AJUTA KURUDISHA KADI YA CHADEMA NA KUINGIA CCM

 Nakaaya leo hii alikuwa kwenye interview ndani ya XXL, katika mengi aliyoyaongea, moja ni kuhusu kurudisha kadi ya Chadema na kuhamia CCM."moja kati vitu  ninavyojutia ni kurudisha kadi ya Chadema na kuingia CCM, najua nimebugi, lakini sio kama watu wanavyoongea kuwa nilipewa hela, kama nilipewa hela si saa hii ningekuwa nakula bata, lakini wapi! mi sijapewa hela.wanajuaje je kama nilitishiwa au vitu vingine kama hivyo..najua hapo nilibugi.Niliingia kwenye siasa kwasababu ya ushawishi wa watu, na nilishawishika kwasababu ya wimbo nilioutoa wakati hui "Mr Politician" lakini baada ya kuingia, niliona kabisa this is not what i can do, siasa ni mchezo mchafu na niliona vinani confuse" amesema Nakaaya kwa picha zaidi


MWIGIZAJI MKONGWE ANUSURIKA BAADA YA KUGONGWA NA GARI

MSANII mkongwe wa filamu Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amegongwa na gari wakati akifanya mazoezi ya kutembea kufuatia ugonjwa wake wa kiharusi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Kariakoo, Dar ambapo gari hilo aina ya Toyota Voxy lilitokea ghafla na kumgonga kidogo na kumsababishia michubuko kwenye miguuni na kichwani.
Dereva wa gari hilo alifanya uungwana kwa kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi ambapo ndugu zake walitaarifiwa na kwenda kumchukua.
“Mzee Kankaa alitoka nyumbani na kutuaga kuwa anakwenda kufanya matembezi. Tulijua ni karibu, lakini baadaye tukasikia taarifa kuwa amepata ajali na yupo Kituo cha Polisi Msimbazi,” alisema Abdul ambaye ni mtoto wa Kankaa.
chanzo : GPL

FFU WAACHA LINDO NA KUINGIA DISCO KUKATA MAUNO


ASKARI Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Kilimanjaro wanaolinda mipaka kukabiliana na biashara za magendo zisiende Kenya, wanadaiwa kuacha lindo na kutinga ukumbi wa disko wakiwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 20 mwaka huu, ambapo askari hao zaidi ya watano waliingia katika ukumbi wa disko wa High Way uliopo njia panda ya Himo na hivyo kutoa mwanya kwa magari sita aina ya Fuso yaliyokuwa yamesheheni sukari ya magendo kupita kirahisi kwenda nchini Kenya.
  
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa baada ya askari hao kutinga katika ukumbi huo, ilichukua muda wa dakika 20 magari yakaanza kupita eneo hilo ambako askari hao walikuwa wameweka doria katika barabara ya Mwika.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS 25.04.2013

9 b8945

1 eeb16
2 3508b

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amwonya Rais kutoipigia debe CCM.


Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) bali afanye kazi za kiserikali.


Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya, Sugu alisema kuwa kitendo hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.


“Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...