Wednesday, May 14, 2014

HII NDIO ORODHA YA WASANII WA KILI TOUR 2014

Ile orodha ya wasanii watakaoshiriki kwenye Kili Music Tour 2014 imetangazwa leo. Kwa mwaka huu zaidi ya wasanii 30 watashiriki katika ziara hiyo kwenye mikoa zaidi ya 10 nchini na itakayoanza ambao Mei hadi Septemba 2014. Wasanii hao ni pamoja na Diamond, Ommy Dimpoz, Linex, Proffesor Jay, Izzo Biznes, Kala Jeremiah, Fid Q, Snura, Weusi, Ben Pol, Mzee Yusuph, Shilole na Mwasiti.
 
Wengine ni Nay wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Juma Nature, Warriors From the East, Madee, Young Killer, Jambo Squad, AY, Vanessa Mdee, Mashujaa Band, Rich Mavoko na Christian Bella. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

HAWA NDIO WATU 10 TANZANIA WANAOTISHA KWA UTAJIRI


 1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). 
Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.

Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.

2. GULAM DEWJI

Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

FERDINAND KUONDOKA OLD TRAFFORD

Mlinzi wa Manchester United Rio Ferdinand amesema ataondoka Old trafford msimu ujao baada ya klabu hiyo kukataa kumuongezea muda kwenye kandarasi yake.
Kauli hiyo inamaanisha Ferdinand ambaye amefunga mabao nane Old Trafford katika miaka 12 na kushiriki katika mechi 454 ataingia katika orodha ndefu ya wachezaji wakongwe mabalozi wa klabu hiyo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa mlinzi huyo anapania kuendelea kucheza lakini haijulikani ataichezea klabu ipi.
pics Rio
Ferdinand kuhama Old Trafford.
Ferdinand alisema katika barua ya wazi kwa klabu hiyo kuwa angelipenda kuwaaaga mashabiki wake kwa njia bora zaidi lakini kutokana na ati ati hangeweza .
Hata hivyo amesema kuwa amefikiria sana kuhusu hatima yake na umewadia wakati wake kuwaaga.
Ferdinand aliwasili United Agosti 2002 kutokea klabu ya Leeds timu hiyo ilipokuwaikikabiliana na Hungary Zalaegerszeg katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Ameshinda mataji 6 ya ligi kuu ya premia mbali na mataji mawili ya nyumbani .
Manchester Utd pia ilishinda taji la klabu bingwa duniani mbali na taji la mabingwa barani Uropa. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: BBCswahili

WACHIMBA MADINI 200 WAFARIKI UTURUKI

157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 200 na kujeruhi wengine wengi kujeruhiwa kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Waziri wa kawi, Taner Yildiz, amesema kuwa zaidi ya wafanyikazi 780 walikuwa katika mgodi huo pale kuliposikika mlipuko katika kitengo cha kusambazia umeme.
Waokoaji wanajaribu kila mbinu kuwafikia mamia ya wachimba migodi.
Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 780 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao .
Bado idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika.
Mgodi huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
157 wameaga dunia katika mkasa wa moto ndani ya mgodi
Jamaa za wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na kububujikwa na machozi.
Waziri wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.
Amesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.
Baadhi yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...