Saturday, December 31, 2016

SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DRC

Wapatanishi wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.

Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.

Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo. 

Mda wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 wamefariki.

TRUMP AMONGEZA PUTIN KWA KUTOLIPIZA KISASI

 
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.

Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.
Lakini katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili mchana. Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.

Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda uchaguzi .

Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya ''ujinga''. Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi. Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...