Wednesday, April 03, 2013

UWOYA NA NDIKUMANA WARUDIANA...ANGALIA PICHA ZAO MBILI WAKIWA KATIKA POZI LA MAHABA


KUNA maswali tena? Ndoa ya staa kiwango cha juu Bongo, Irene Uwoya na mumewe Hamad Ndikumana 'Kataut' anayeng'ara katika kabumbu akikipiga pande za Rwanda imerejewa na uhai tena..

BREAKING NEWzzzzzzzzzzzzzzz!!!! MPAKA WA TUNDUMA MBEYA WAFUNGWA KWA MUDA POLISI WATUMIA MABOMU

 
kamanda  wa polisi  wa mkoa  wa Mbeya  Diwani Athuman 

Taarifa  kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Mwandishi  kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa  vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana  kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati wa pasaka.

WEMA SEPETU AAMUA KUMUENZI MCHINA WAKE KWA KUJITANDIKA TATTOO ZA KICHINA SHINGONI NA MGONGONI


PINDA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU

 

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha  kutokana na  kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la Moshono, Arusha. 

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za uchimbaji katika eneo hilo.

Hatua hiyo ya Pinda imetokana na ajali ya watu 14 waliopoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi juzi, wakati wengine wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na mvua zinazonyesha jijini Arusha.
Pinda alitoa agizo hilo alipotembelea eneo hilo pamoja na kuwajulia hali majeruhi wawili waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mt Meru
CHANZO:MWANANHI.

KAJALA AMLIPA FADHILA WEMA

Siku chache baada ya kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipiwa faini ya sh. Millioni 13 mwanadada wa bongo movie Kajala Masanja kaamua kumlipa fadhira ya kuchora tatoo yenye jina la msanii mwenzake Wema Sepetu ambae ndie aliemlipia kiasi hicho cha fedha na kumfanya kuwa huru tena.










jambotz8.blogspot.com

MAGAZETI YA LEO APRIL 3, 2013

DSC03777DSC03778
DSC03775 

DSC03776

LOWASSA AMTOA KAFARA PINDA

WABUNGE WAUNGANISHA NGUVU KUTAKA KUMSULUBU BUNGENI





RIPOTI ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka 2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam, imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Pinda anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Kutokana na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa chini ya kiwango.

KANGAMOKO WATIA AIBU TENA MKOANI KAGERA HEBU ANGALIA PICHA HIZI




SUMATRA YATANGAZA KUPANDA KWA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU NA DALADALA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

IMG_6840Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya taasisi hiyo wakati akitangaza kupanda kwa viwango vya nauli ya mabasi ya mikoani na Daladala.
………………………………………………………………..

 Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...