Friday, June 06, 2014

WARIOBA AZISHUKIA UKAWA NA CCM


Katika Bunge hilo, wajumbe wengi wa CCM walimshambulia Warioba na tume yake wakidai kuwa Rasimu ya Pili ya Katiba haikuzingatia maoni ya wananchi na Mabaraza ya Katiba. PICHA|MAKTABA 

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashauri wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na CCM kuacha kuzunguka mikoani kufanya mikutano inayoeleza misimamo yao kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa haina tija kwa taifa.
Ameonya kuwa mikutano hiyo inajenga mwelekeo mbaya kwa taifa na kuhatarisha mchakato wa Katiba na kuzitaka pande hizo kumaliza tofauti zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika Dar es Salaam jana, Warioba alisema: “Kwa mustakabali mwema wa taifa, ni muhimu makundi haya ‘ya-resolve’ (yamalize), matatizo yaliyopo kabla ya Agosti, ili Bunge Maalumu la Katiba likirejea, wote washiriki na kukamilisha mchakato wa kupata Katiba Mpya. Hili ni kwa masilahi ya taifa.”
Kauli ya Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu, imekuja huku makundi ya Ukawa linaloundwa na wabunge wengi wa upinzani na viongozi wa CCM wakiendelea kung’ang’ania misimamo yao kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati CCM ikipinga mapendekezo ya kuwapo kwa mfumo wa serikali tatu uliomo kwenye Rasimu, Ukawa unaunga mkono mapendekezo hayo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TIGO, AIRTEL NA ZANTEL ZAUNGANISHA HUDUMA




Meneja Mkuu wa Kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez (Kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Muhula wakitia saini ya makubaliano jijini Dar es Salaam jana baina ya Tigo na DTBi ya kusaidia wajasiriamali kujifunza teknolojia ya digitali na mawasiliano. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Hassan Mshinda. Picha na Venance Nestory.


Kampuni za simu za mkononi za Tigo, Airtel na Zantel zimeunganisha huduma zao za kutoa, kutuma na kuweka fedha na sasa mteja anaweza kutuma fedha kutoka mtandao mmoja kupitia mwingine.

Taarifa ya pamoja na kampuni hizo iliyotolewa jana, ilisema kuwa wote wanaotumia huduma za kifedha za mitandao hiyo, wataweza kutumiana fedha kupitia simu zao za mikononi pasi na tatizo baada ya kampuni hizo kuunganisha huduma zao.

Huduma hiyo inayotarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu, itawafanya wateja wa mitandao hiyo kutumiana na kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao tofauti na ilivyokuwa awali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MTAWA WA KANISA KATOLIKI ASHINDA KATIKA SHINDANO LA KUIMBA...!!!

Mtawa wa Italia anyakua ushindi
Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo. Mtawa huyo, Sister Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki shindano la The Voice.
Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika ushindi huo. Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One', umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.
Mtawa huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu wa kawaida. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC Swahili

DRC YAILAUMU RWANDA KWA KUWALINDA M23




DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeikashifu serikali ya Rwanda kwa kuwalinda wapiganaji wanaotuhumiwa kwa kusababisha mauaji ya halaiki chini ya nembo ya wapiganaji wa M23.
Afisa mmoja wa Serikali ya DRC ameiambia BBC kuwa imekuwa vigumu kwa serikali yake kuwahoji zaidi ya wapiganaji 500 ambao wamekita kambi nchini Rwanda licha yao kutuma ombi la kufanya hivyo yapata miezi saba iliyopita . Zaidi ya watu 800,000 walitoroka makwao haswa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo wakati wa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe.

Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo na kusema kuwa imeshirikiana na serikali ya DRC. Kundi hilo la M23 lichukua silaha mashariki mwa DRC kuanzia Aprili 2012, liliaumu serikali ya Kinshasa kwa kuwabagua jamii ya watutsi na pia kupuuza makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano. Kundi hilo hata hivyo lilishindwa katika mapigano yaliyoongozwa na jeshi la Umoja wa mataifa likisaidiwa na majeshi ya serikali ya Congo mnamo November 2013. Wapiganaji hao walitorokea Rwanda na Uganda.


DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Katika mji wa Ngoma, mashariki mwa Rwanda mwandishi wetu alikumbana na wapiganaji hao ana kwa ana katika kambi nje ya mji. Wengi wao wanasema kuwa wamechoshwa na ngoja ngoja hiyo ambayo imedumu kwa kipindi kirefu sasa na wanasema kuwa wangependa kuomba hifadhi nchini Rwanda, kwani wanahofia kurejea ndani ya Congo.
 Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali ya Congo imetangaza kuwa itawapa msamaha wapiganaji hao. Tulipoingia ndani ya kambi hiyo ,hali na taswira ilikuwa tulivu na shwari. Kulikuwa na hema kubwa nyeupe, majengo kadha mbali na bustani iliyolindwa na nadhifu. Wapiganaji hao wanalala sita katika chumba kimoja .

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...