Saturday, April 06, 2013

MSANII WA BONGO FLEVA AFARIKI DUNIA KWA KUJIDUNGA SINDANO ZA MADAWA YA KULEVYA....!!

MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya aliyetambulika kwa jina moja la Rocky mkazi wa Kawe, Dar amefariki dunia baada ya kujidunga madawa ya kulevya.


Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia tukio hilo na kuomba hifadhi ya jina lake, marehemu anayekadiriwa kuwa na umri wa
Ray C

AFUNGWA MIAKA 10 JELA KWA KOSA LA "KUMPIGA DENDA" NA KUMTOMASA UKENI BINTI WA MIAKA 13 HUKO MPANDA

MAHAKAMA Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41) mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa yake.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Awali katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mtoto huyo alikuwa akitoka shuleni akielekea nyumbani kwao ndipo mshitakiwa alipoona anapita karibu ya nyumba yake ambapo alimwita msichana huyo na kisha alimwingiza kwa nguvu nyumbani kwake.

TANZANIA YAONGOZA KWA UNYWAJI WA POMBE ZA KIENYEJI (MATAPUTAPU)

Pombe ya kienyeji ikiandaliwa tayari kupelekwa kwa walaji 

UTAFITI wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.

Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52, ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.

Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.

HUYU NDO BIBI ANAYEDAI KUISIKIA SAUTI YA MUNGU

Amani usiamini! Bibi kizee Veronica Amos Kayombo (76), mwenyeji wa Ludewa, Njombe anayeishi Buza, Dar, amedai kuisikia sauti ya Mungu ikimuagiza akaonane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ampe ujumbe muhimu, shuka nayo.

MAHOJIANO MAALUM

Akizungumza katika mahojiano maalum mwanzoni mwa wiki hii akiwa nyumbani kwake Buza, Bibi Veronica alisema amekuwa akitokewa na Mungu mara kwa mara na kumpa maelekezo mengi ambayo anatakiwa kuyatoa pale atakapofika kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.

AUNT EZEKIEL ANASWA NDANI YA POZI LA NUSU UCHI UKUMBINI

Kweli sikio la kufa halisikii dawa! Licha kuolewa na Sunday Demonte, msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ametia aibu kwa mara nyingine tena baada ya kunaswa nusu utupu ukumbini usiku wa manane.
  

Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilijiri juzikati katika Ukumbi wa Nyumbani, mjini hapa ambapo Aunt aliwashangaza mashabiki waliofurika kwenye shoo ya Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Aunt alivaa kipensi kilichoacha mapaja yote wazi hadi kulazimika kujifunika kwa pochi na kitopu ‘transiparenti’ kilichoonesha kila kitu hadi ‘chakula ya mtoto’.

Zanzibar yapiga marufuku ndoa za jinsia moja.

Mhe. Abubakar Khamis Bakar, Waziri wa Katiba na Sheria wa ZanzibarMhe. Abubakar Khamis Bakar, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu jinsia moja.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).
 
Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu.

Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.
Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 06.04.2013

.
.
.
.

DIAMOND, OMMY DIMPOZ WAPIGANA VIJEMBE KWENYE TWITTER...!!

Mapema leo, Diamond Platnumz ali-tweet kupitia ukurasa wake wa Twitter kuhusu mambo ya mapenzi na mahusiano ...
In between, Ommy Dimpoz jumped in... This is too far hilarious ... Ha ha ha ...
Ni kweli haya yanatokea??!!
Check them tweets hapa chini :

MACHANGUDOA WA RWANDA WAZITIKISA NDOA ZA WABUNGE, WAKE ZAO WAHOFIA KUAMBUKIZWA UKIMWI....!!

Ndoa za baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinadaiwa kuwaka moto kufuatia kuibuka kwa wimbi la madadapoa raia wa Rwanda ambao wamekiri kuwapa uroda waheshimiwa hao wanapokuwa mjengoni, Dodoma,Uchunguzi umebaini kuwa, wake wa waheshimiwa hao walipata mshtuko mkubwa hivi karibuni kufuatia taarifa ya kukamatwa kwa machangudoa hao, Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera (25) huku wawili kati yao wakikutwa na dawa za kupunguza makali ya Virusi Vya Ukimwi (ARVs).
 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...