MAHAKAMA
Hakimu ya Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu Kassim Lugendo (41)
mkazi wa kijiji cha Kambanga tarafa ya Kabungu kifungo cha miaka 10 jela
kwa kosa la kumnyonya ulimi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13,
anayesoma darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula, bila ridhaa
yake.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Chiganga Tengwa alitoa hukumu hiyo
jana baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali
katika kesi hiyo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi wa Polisi, Ally Mbwijo
aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa Lugendo alitenda kosa hilo Machi
30 mwaka jana, saa sita mchana akiwa nyumbani kwake.
Mbwijo
aliiambia mahakama kuwa, baada ya mshitakiwa kumwingiza ndani ya nyumba
yake msichana huyo, alianza kumnyonya ulimi kwa nguvu huku akimtomasa
sehemu za siri kwa vidole.
Ilielezwa
mahakamani hapo kuwa wakati akimfanyia uovu huo, mtoto huyo alikuwa
akiomba msaada kwa kupiga kelele muda ambapo majirani walifika eneo la
tukio na kumkuta mshitakiwa akiwa ameshaanza kumvuta mtoto huyo sketi
yake ya shule.
Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulileta mahakamani hapo mashahidi watatu na mshitakiwa hakuwa na shahidi yeyote.
Akijitetea,
Lugendo aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile alichokieleza kuwa
yeye ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote wawili ni walemavu,
hivyo ana watu wengi wanaomtegemea.
Hata
hivyo, Hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha
kinyama na hatari kwani kina weza kumsababishia mtoto huyo ugonjwa wa
ukimwi. Alimtia hatiani na kumwadhibu kifungo cha miaka kumi jela.NA
MPEKUZI

No comments:
Post a Comment