Pombe ya kienyeji ikiandaliwa tayari kupelekwa kwa walaji
UTAFITI wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).
Utafiti
huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa
pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda
kwa asilimia 6.44.
Kwa
mujibu wa utafiti huo, Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na
asilimia 4.52, ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.
Ivory
Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania
ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake
kunywa pombe chafu.
Ripoti
ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda
kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.
Mtaalamu
wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha
Figo, Dk Francis Fulia aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo kwa
sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama.
Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao.
“Watanzania
waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia
sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,
moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza.
Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.
“Pombe
haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo, inatumika katika
kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” alisema.
Aliongeza
kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa
kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika
vituo mbalimbali vya afya.
Katika
miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza
katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo
gongo na pombe nyingine.
No comments:
Post a Comment