Friday, November 28, 2014

ASKOFU KILAINI, NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA YA ESCROW

Baba Askofu Methodius Kilaini  

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni). Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ESCROW NJIAPANDA, WABUNGE WAGAWANYIKA...!!!




Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati)  akiwasihi Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa  Nkasi, Ali Kessy wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.

Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.

Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.

Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 28, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
;
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

IKULU YAHUSISHWA NA ESCROW

Ikulu ya rais nchini Tanzania 
 
Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.

WANAUME 13 WASHTAKIWA KWA UDHALILISHAJI

Genge la Wanaume waliotekeleza vitendo vya udhalilishaji dhidi ya Wasichana 
 
Wanaume kumi na watatu wameshtakiwa kwa kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji kwa Watoto mjini Bristol, ikiwemo vitendo vya ubakaji na kuwalazimisha watoto wa kike kujiingiza kwenye vitendo vya biashara ya ngono.
Mahakama ya mjini Bristol ilimsikiliza binti wa miaka 16 aliyebakwa na Wanaume watano raia wa kisomali.
Halikadhalika mdogo wake mwenye umri wa miaka 14 alibakwa na mmoja wa wanaume hao, Msichana huyo alipofika kumtembelea Dada yake.
Uchunguzi uliofanywa na Polisi ulibaini kuwa genge jingine la wanaume wenye asili ya kisomali liliwadhalilisha kijinsia wasichana wengine wanne.
Wasichana hao walilipwa pauni 30,au kupewa dawa za kulevya, vilevi na zawadi kwa ajili ya kushiriki vitendo vya ngono na wanaume wenye umri mkubwa wa jamii ya kisomali.
Miongoni mwa walioshtakiwa ,Watu sita walihukumiwa kifungo,wengine saba walitiwa hatiani siku ya jumatano. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

WAFANYABIASHARA WA UGANDA WAIONYA KENYA

Wafanyibiashara wa Uganda wameonya kuihama bandari ya Mombasa kutokana na ada mpya za mara kwa mara. 
 
Wafanyibiashara wa Uganda chini ya muungano wa Wanabiashara wa mji wa Kampala Uganda KACITA wamelipa Shirika la ukusanyaji Ushuru nchini kenya KRA wiki mbili kuitoa mizingo yote inayoelekea Uganda la sivyo waigomee bandari ya Mombasa.
Ilani hiyo iliafikiwa siku ya Alhamisi baada ya saa kadhaa za majadiliano kuhusu athari za hatua ya KRA ya kutoza kodi bidhaa zote zinazoingia katika badari hiyo.
Awali ,wafanyibiashara walikuwa wakilipa ada wanayotozwa wakati wanapochukua mizigo yao pamoja na ada nyenginezo.
Hatua hiyo kulingana na KACITA si kinyume na matarajio ya jumuiya ya Afrika mashariki pekee bali pia inawaumiza wafanyibiashara wa Uganda pamoja na uchumi.
Mwenyekiti wa KACITA Everest kayondo amesema kuwa kufikia jumatano kulikuwa na makasha 4,000 yanayozuiliwa katika Bandari ya Mombasa kutokana na ada za mara kwa mara zinazotolewa na KRA.
''Kwa hivyo tunaipa KRA wiki mbili kutoa mizigo yote ya Uganda la sivyo tuhame hadi katika bandari ya Dar es Salaam'',.aliongezea
Wafanyibiashara hao pia walikubaliana kwamba iwapo mahitaji yao hayataafikiwa ,wataishinikiza serikali ya Uganda kuzuia bidhaa za kenya zinazoingia katika soko la Uganda. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PHILIP HUGHES AFARIKI DUNIA

Philip Hughes
Bendera zinapepea nusu mlingoti katika viwanja vya cricket nchini Australia katika kuomboleza kifo cha mcheza crickte Philip Hughes aliyefariki hapo jana baada ya kupigwa na mpira. Salaam za rambi rambi zimeendelea kutolewa kutoka sehemu mbali mbali duniani. Baadhi ya wachazaji wa cricket wamekuwa wakiacha magongo ya mchezo huo katika mlangoni mwa nyumba zao kama ishara ya kuomboleza kifo hicho. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...