Sunday, June 08, 2014

TANZIA: MZEE SMALL AFARIKI DUNIA

1_e4ab8.jpg
Mzee Small enzi za uhai wake.
Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku huu akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar. Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili. Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha Mzee Small. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 08, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

..
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI ILIVYOFANA



2_31d12.jpg
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari jana amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza saa 7:00 mchana  ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga 'mpunga' wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema 'Nassari ameacha historia'. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
CHANZO: Mitandao ya Kijamii.

RAIS MPYA WA MISRI KUAPISHWA

Raia wanaomuunga mkono Abdel Fatah al sisi
Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Abdel Fatah el Sisi.
Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo.
Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...