Monday, March 26, 2018

MAGUFULI AZINDUA MAGARI 181 YA BOHARI KUU YA DAWA (MSD)

Rais Magufuli akiwasili Bohari kuu ya Madawa (MSD) Jijini Dar es salaam kabla ya kuzindua magari  181, Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu,Mwakilishi wa Taasisi ya Global Fund Bw. Linden Morrison na viongozi wengine.Machi 26,2018.
  

SIMBA NA YANGA KUKUTANA TAREHE HII HAPA

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu, Boniface Wambura leo imetangaza rasmi tarehe ambayo Watani wa Jadi (Simba SC na Yanga SC) watakutana kucheza mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

  Wambura amesema timu hizo sasa zitacheza tarehe 29 Aprili 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ambayo Simba atakuwa mwenyeji wa pambano hilo. Awali Bodi ya Ligi ilikuwa haijaweka tarehe hiyo wazi kutokana na mambo mbalimbali kuingiliana na kufanya ratiba ya mchezo huo kutopangwa kwa wakati.

Timu hizi zenye wafuasi wengi nchini, zilikutana Oktoba 28 2017 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi na kwenda sare ya bao 1-1, huku wafungaji wa mabao hayo wakiwa ni Shiza Kichuya upande wa Simba na Obrey Chirwa kwa Yanga.

Pamoja na michezo mingine mbalimbali ambayo leo imetolewa ratiba yake rasmi, klabu ya Simba imepangwa kucheza;

Njombe Mji FC Vs Simba April 3
Mtibwa vs Simba Aprili 9
Lipuli FC vs Simba Aprili 20
Simba vs Yanga Aprili 29

NONDO AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa leo Jumatatu, Machi 26, imemuachia Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP), Abdul Nondo kwa dhamana ya Sh. 5 milioni na mali isiyohamishika.

Nondo amepewa dhamana hiyo mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia anayeendesha kesi hiyo baada ya mtuhumiwa kukamilisha taratibu zote za dhamana.

Wiki iliyopita, Nondo alinyimwa dhamana baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa ni kwa sababu za usalama wake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...