Friday, April 05, 2013

CHEK LIST YA WASANII WATAKAO PERFORM SHEREHE ZA KUAPISHWA RAISI UHURU KENYATA

Jana nilitoa baadhi ya majina ya wasanii waliotajwa kuperfom kwenye sherehe za kuapishwa kwa Raisi mpya wa Kenya , Kenyata, leo hii nimepokea list kamili ya wasanii watakaoshiriki na safari hii Jaguar hakuachwa nyuma.
 
List hiyo ni Daddy Owen, Jaguar, Emmy Kosgey, Rufftone, Ringtone, Abass, V6, Sauti Sol, Sarakasi Dancers, Madtraxx, ambao watu wengi walikuwa wakitegemea kuona list ya majina haya.

 
wengine ni pamoja na Elsie na Visita, walioimba wimbo wa jubilee, pamoja na Ally B, Gkon na  Kavi Pratt.its more about music industry and social issues in and out of bongo land

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiongozwa na Askari polisi kuingia katika Mahakama Kuu ya Zanzibar  kusikiliza kesi inayomkabili.
 wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) kulia akizungumza na mawakili wake Abdalla Juma kushoto na Rajab Abdalla muda mfupi baada ya kutajwa kwa kesi yake Mahakamani hapo. 
 Mawakili wanaomtetea Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri , Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) wakili Abdalla Juma (kulia) na Rajab Abdalla wakiwa mezani pao  kabla ya kutajwa kwa kesi ya mteja wao katika mahakama Kuu Vuga mjini Zanzibar
Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake kutajwa mahakamani hapo.
 Picha zote na Haroub Hussein

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Justice Ernest Mwipopo, aliyefariki kwa ajali ya gari April 3, huko maeneo ya Morogoro. Shughuli hizo za kuaga mwili huo zimefanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya shughuli hizo mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko kesho.
 Mmoja wa majaji akibeba picha ya marehemu wakati majaji hao wakishuha jeneza hilo lenye mwili wa marehemu, ili kuanza shughuli za kuaga katika viwanja vya Karimjee leo.

MZEE MANGULA KUFUNGA NDOA NA MKUU WA SHULE YENYE JINA LAKE


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula anatarajia kufunga ndoa kesho katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, mjini Njombe.
Mzee Mangula anafunga ndoa na Mkuu wa Sekondari ya Philip Mangula, iliyopo wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, Yolanda Kaberege.


Hatua hiyo ya Mzee Mangula kuoa inakuja baada ya aliyekuwa mke wake kufariki dunia mwaka 2004, kutokana na ugonjwa wa saratani.

Msemaji wa familia ya Mzee Mangula ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tawi la Njombe, Dk Lechion Kilimike alilieleza Mwananchi kuwa ndoa hiyo itaongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa hilo, Solomon Swalo.

MAGAZETI YA LEO APRIL 5, 2013


6 6b9aa

3 17596

4 af0df

KAJALA APEWA SHAVU JINGINE NA WEMA...........!!!!



Muigizaji na Miss Tanzania wa zamani Wema Sepetu amesema licha ya kumsainisha Kajala Masanja kwenye kampuni yake, hategemei kumfanyisha kazi kurudisha shilingi milioni 13 alizomtolea kwenye hukumu yake.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, Wema amesema Kajala atakuwa akifanya kazi zake lakini atakuwa akimlipa kama kawaida. Kwa kuanza Kajala ataigiza kama mhusika mkuu kwenye filamu iitwayo Princess Sasha.
“Tutaenda kuishoot nje ya Dar, ninataka kuishoot mandhari fulani hivi kama ya kijijini. Ni mtoto wa mfalme, Kajala ndo atakuwa Princess Sasha, she is going to be the main character, “ alisema Wema.
Kajla

DAWA MPYA ZA KIENYEJI ZA KUKUZA MAKALIO ZAWATEKA WAREMBO WENGI

BAADA ya zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti zilizotikisa Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji


Uchunguzi uliofanywa na audifacejackson blog kupitia kwa wataalam mbalimbali wa tiba za asili TANZANIA , ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa waganga wa kienyeji.

KAJALA, WEMA NA PREZZO WAFUMWA WAKILA BATA MAENEO

Wema katika pose na Prezzo  & don't get it twisted guys hii ilikuwa kikazi zaidi
Prezzo akishow love kwa warembo wetu Kajala & Wema
Wamependeza eeee??

JOKATE KUKITANGAZA KIMATAIFA KIKUNDI CHA WANAHABARI


Aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006 Jokate Mwegelo alijitolea kuwafungulia website kikundi hicho ili kiweze kujitangaza na kutambulika ndani na nje ya nchi.

Jokate alisema kuwa ili kikundi hicho kifanikiwe ni lazima wajitambue na kuwe na timu imara ambayo itakuwa makini na nia thabiti ya kujiinua kimaisha na kukuza uchumi wa Taifa.

"Mafanikio niliyokuwa nayo si kwasababu mimi ni bilionea bali ni kutokana na ushirikiano tuliokuwa nao mimi na wenzangu hadi tukafanikiwa kuwa na kampuni inayojulikana kama kidoti". Alisema Jokate.

Aliongeza kuwa japo kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali lakini wanaendelea vizuri na biashara ambapo mbali na kuuza nywele tunatarajia kuuza vipodozi pamoja na nguo

Mbali na hilo alisema kuwa ili wafanikiwe ni lazima wawe na upendo ili kila mtu aweze kuwa huru na kueleza kile anachokiona kina manufaa katika kikundi.

Tigo yadhamini Ngorongoro Marathoni

Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo imedhamini Mbio za Sita za Ngorongoro Marathon zenye lengo la kupambana na ugonjwa wa malaria zinazotarajiwa ‘kutimua vumbi’jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu  katika mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Ufunguzi wa mbio hizo utafanywa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu.

Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kuwa, kwa mwaka huu kampuni hiyo imetoa  fedha taslimu, simu za kisasa kabisa za mkonaoni pamoja na muda wa hewani kwa mshindi wa kwanza wa kundi la wanaume na mshindi wa kwanza kwa kundi la wanawake.

“Tigo kwa kuwajali Watanzania, tumeona umuhimu mkubwa sana wa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambapo dhidi ya malaria ambayo imekuwa ikipoteza maisha ya watu wengi wa rika mbalimbali kupitia mbio hizi…” alifafnua Mpinga. Kwa upande wake Mratibu wa ZARA Charity ambao ndio waandaji wa mbio hizo Bw, Datus Joseph alifafanua kuwa, pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya malaria, mbio za Ngorongoro Marathon pia zinasaidia kukuza utalii wa ndani na nje ya nchi.

“Mbio hizi ni za Sita tangu kuanzishwa kwake na Tigo wameendeea kutupa ‘support’ na tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa wadhamini wetu…” alifafanua Joseph. Aliendelea kufafanua kuwa, ZARA Charity inawashukuru wadhamini mbalimbali wa mbio hizo ambazo zimekuwa za mafaniko makubwa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...