BAADA
ya zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti
zilizotikisa Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’
moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili
kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji
Uchunguzi
uliofanywa na audifacejackson blog kupitia kwa wataalam mbalimbali wa
tiba za asili TANZANIA , ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa
waganga wa kienyeji.
Ilifahamika
pia kuwa hivi sasa dawa hizo zinachangamkiwa na wanawake ile mbaya
wakiamini kwamba hazina madhara kama zile za Kichina.
NI MCHANGANYIKO WA MITI 60
Mmoja
wa wataalam hao aliyezungumza na audifacejackson blogalisema kuwa, dawa
hiyo ni mjumuisho au mchanganyiko wa miti zaidi ya 60 inayopatikana
kwenye misitu mikubwa hasa mikoani.
JINA LAKE
audifacejackson blog jina la dawa hiyo, mtaalam huyo alisisitiza:“Nimeshakuambia
ni mchanganyiko wa miti zaidi ya 60, haina jina isipokuwa mteja akifika
anatakiwa aseme kama anataka mzigo wa saizi gani.”
UNACHAGUA KALIO UNALOTAKA
Mtaalam
huyo alikwenda mbele zaidi na kuweka kweupe kuwa dawa hiyo ni kiboko ya
Mchina kwani dozi na bei yake hutegemea aina ya kalio analolitaka mteja
husika.
“Ukitaka dogo, la kati au kubwa, kila moja lina dozi na bei yake hivyo inategemea mteja amechagua la aina gani,” alisema mtaalam huyo. WATAALAM WA TIBA ASILIA WANASEMAJE?
waandishi
wa audifacejackson blog waliendelea kufanya mahojiano na wataalam
mbalimbali wa tiba za asili ambapo walikuwa na haya ya kusema:
MJUKUU WA BABU
Mganga maarufu kwa jina la Mjukuu wa Babu anayepatikana Mwananyamala jijini Dar es Salaam alifunguka:
“Nakwambia
hii dawa ni kiboko ya zile za Kichina. Ni dawa nzuri na kusema kweli
watumiaji ni wengi. Ni mchanganyiko wa miti zaidi ya sitini ambao huwa
unatoa aina moja ya dawa.
No comments:
Post a Comment