Tuesday, June 17, 2014

CHENGE: "SERIKALI IMEKOSA UBUNIFU"


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge. PICHA|MAKTABA 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge amesema Serikali imekosa ubunifu na haitaki kupokea ushauri kuhusiana na vyanzo vipya vya mapato ya uchumi kwa mwaka 2013, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/15 pamoja na utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2013/14, Chenge alisema kuongeza ushuru katika bia, soda, juisi na vinywaji vikali, kumepitwa na wakati.

Wakati Chenge akieleza hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetaja vyanzo mbadala vya mapato vinavyofikia Sh6 trilioni. Katika taarifa yake, Chenge alisema mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2013/14, Bajeti ilikuwa pungufu kwa Sh2 trilioni, huku Bajeti ya mwaka 2014/15 ikiongezeka kwa asilimia 8.8 (trilioni 1.6), huku ikiwa na deni la Sh1.3 trilioni ambalo halikuingizwa katika Bajeti ya mwaka 2014/15.
“Hali hii inaweza kutafsiriwa kuwa Bajeti ya mwaka 2014/15 tayari ina pengo la Sh4.9 trilioni. Yaani Sh2 trilioni ambazo hazikupatikana mwaka wa fedha 2013/14 na Sh1.6 trilioni ambayo imeongezeka ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana na deni la Sh1.3 trilioni.
“Kuna umuhimu wa kuharakishwa kuletwa bungeni sheria ya bajeti itakayofanya kazi sambamba na sheria mpya ya ununuzi ili kudhibiti matumizi mabaya kwa nia ya kuweka nidhamu katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali,” alisema Chenge. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWANAMUZIKI APASULIWA HUKU AKIIMBA...!!!

Alama Kante afanyiwa upasuaji
Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba. Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.

Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea. Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa kote duniani.

Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote. 
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI KUTUMA MAJESHI IRAQ

majeshi ya marekani Iraq

Marekani imetangaza kuwa inatuma wanajeshi 275 nchini Iraq kusaidia kulinda maafisa na Ubalozi wake mjini Bagdad. Tangazo hilo limetolewa wakati maafisa wa Marekani na Iran wakifanya mazungumzo kuhusu hali nchini Iraq katika kongamano linalojadili maswala ya nyuklia mjini Viena.

Rais Obama ameandika barua kwa baraza la Congress kueleza mipango ya kutuma wanajeshi hao 275 mjini Baghdad. Anasema jukumu la kikosi hicho ambacho kitakabidhiwa silaha ni kulinda raia wa Marekani wanaoishi nchini Iraq na mali yao. Wanajeshi hao wataendelea kukaa nchini humo hadi hali ya usalama itakapoimarika.

Hatahivyo hakuna ishara yoyote ya hali kuimarika huku kundi la wapiganaji la ISIS likiendeleza harakati zake katika baadhi ya maeneo ya Iraq. Rais Obama ambaye anaonekana kutafakari kuhusu hatua ambazo Marekani inaweza kuchukua, anashauriwa na maafisa kutoka kitengo cha usalama wa kitaifa. Kwingineko maafisa wa Marekani wamethibitisha kuwa wamefanya mazungumzo mafupi na maafisa kutoka Iran kuhusu hali nchini Iraq.

Awali waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry alisema yuko tayari kushauriana na Iran ambayo wakati mmoja ilikua hasimu wa Marekani. Hatahivyo maafisa wa Marekani wametupilia mbali uwezekano wa ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Chanzo BBC

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HIVI NDIVYO RADIO COUNTRY FM ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA

Wafanyakazi wa radio country fm wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kitu cha watoto wenye ulemavu wa viungo cha SAMBAMBA kilichopo Kitwiru
Kaimu meneja wa Radio Country fm Chiku Mbilinyi akimkabidhi diwani wa kati ya kitwiru zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu
kaimu meneja wa radio country fm CHIKU akimkabidhi mratibu wa kituo hicho zawadi kwa ajiri ya watoto wenye ulemavu
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE ATETA NA WASANII DODOMA

D92A1853Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisistiza jambo wakati akizungumza na msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul “Diamond” ikulu ndogo mjini Dodoma wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi.Kulia ni mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.D92A1860Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na msanii wa kizazi kipya Nasib Abdul “Diamond” ikulu ndogo mjini Dodoma wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi.Kulia ni mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.D92A1891Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanamuziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi iliyopita kulia ni Mh. Ridhiwani Kikwete Mbunge wa jimbo la Chalinze(picha na Freddy Maro). Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

URENO YA RONALDO YALA KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA KWA `WANYAMA` UJERUMANI

article-2659215-1ED2CD1400000578-919_634x442
Wachezaji wa Ujerumani wakumpongeza mwenzao Thomas Muller (kushoto) baada ya kupiga hat-trick leo
MJERUMANI Thomas Muller awa mchezaji wa kwanza  kufunga mabao matatu katika mechi moja `hat-trick`  kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil baada ya kuiongoza nchi yake kuilaza Ureno mabao 4-0 usiku huu mjini Salvador. Nyota huyo wa Bayern Munich alifunga bao la kuongoza dakika za mapema kwa mkwaju wa penati na kuwapa mwanzo mzuri katika uwanja wa Arena Fonte Nova wana nusu fainali hao wa mwaka 2010 nchini Afrika kusini. 
Mabao ya Muller usiku huu yalifungwa katika dakika za  12 (penati), 45, 78, na goli lingine lilifungwa na beki wa kati Mats Hummels katika dakika 32 Ureno walipata majanga baada ya mshambuliaji wake wa kati Hugo Almeida na Fabio Coentrao kupata majeruhi, lakini mbaya zaidi walishuhudia  beki wao wa kati Pepe  akitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu yake iko nyuma kwa mabao 2-0 baada ya kumfanyiwa madhambi Muller. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...