Tuesday, June 17, 2014

MWANAMUZIKI APASULIWA HUKU AKIIMBA...!!!

Alama Kante afanyiwa upasuaji
Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba. Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.

Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea. Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa kote duniani.

Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote. 
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...