Friday, September 27, 2013

MJUE GAIDI SAMANTHA ALYEONGOZA AL-SHABAAB KUUA KENYA


Samantha20Lewthwaite-9559681 1f85a 
Adaiwa kuuawa Westgate
*Alifika Tanzania kwa Pasipoti ya Afrika Kusini
Ssamantha Lewthwaite, mwanamke wa Uingereza anayetajwa kuwa kiongozi wa ugaidi uliofanyika Nairobi, Kenya

WAKATI umwagaji wa damu katika kituo cha biashara cha Westgate ukiingia siku ya nne jana, Mwanamke ambaye ni raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite (29), anayetajwa kuwa ndiye aliyeongoza kundi la Al-Shabab kufanya shambulizi hilo, anahofiwa kuuawa.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza, lilikariri vyanzo vyake vilivyoko ndani ya Jeshi na mfumo wa usalama nchini Kenya, ambavyo vimethibitisha kuwa mwanamke huyo ni miongoni mwa magaidi waliouawa na Serikali ya Kenya.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, katika mahojiano yake na kituo cha habari cha PBS, hakusema kama mwanamke huyo ameuawa lakini alithibitisha kuwa miongoni mwa magaidi waliovamia Westgate ni mwanamke wa Uingereza ambaye hata hivyo hakumtaja jina.
Hatua hiyo iliibua tetesi kwenye vyombo vya habari vya Kenya ambavyo vilimtaja mwanamke huyo kuwa ni Samantha.
Hata hivyo kauli hiyo ya Waziri huyo inaonekana kupingana na ile iliyotolewa awali na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, ambaye alisema kuwa magaidi wote waliovamia kituo hicho walikuwa wanaume na kwamba huenda baadhi yao walivalia mavazi ya kike.

TAARIFA YA JKT KWA VIJANA WANAOTAKA KUAHIRISHA MAFUNZO

JKT1_4a456.jpg
Vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT awamu ya tatu na pia wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu, wambao wanataka kuahirisha mkataba wa JKT, wanatakiwa kuandika barua Makao Makuu ya JKT kuomba kuahirisha mkataba wa JKT.
1. Barua binafsi kuomba kuahirisha mkataba iwe na picha yake.
2. Nakala ya barua ya kucahguilwa kujiunga na chuo (Joining instructions)
3. Barua hiyo ieleze kuwa utajiunga na JKT baada ya kuhitimu masomo.
4. Barua zao zifike Makao Makuu ya JKT kabla ya tarehe 02 Kotoba, 2013.
ANGALIZO
Kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Hivyo ni wajibu wa kila mhitimu kuhudhuria mafunzo hayo.
Agizo hili limetolewa na Jeshi la Kujenga Tafia, Makao Makuu.
---
Imetolewa kwenye tovuti: http://jkt.go.tz/mkataba-jkt.html

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2g4C18z5v

KENYA YAMSAKA SAMANTHA LEWTHWAITE

nairobi c0494
Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa sana duniani.
Hatua hii ni kutokana na ombi la serikali ya Kenya kwa Interpol.
Bi Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, ni mjane wa mlipuaji aliyefanya shambulizi la kujitoa mhanga mjini London Uingereza mwezi Julai mwaka 2005
Anajulikana kama "white widow", na amehusishwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab nchini Somalia.
Polisi wa Interpol hata hivyo hawakuhusisha hatua ya kumsaka Samantha na shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi lililowaua watu 67.
Hata hivyo, hatua hii ya kumsaka Bi Lewthwaite inakuja punde baada ya shambulizi hili la kigaidi nchini Kenya.
Al-Shabab ilikiri kufanya mashambulizi hayo yaliyotokana na kutekwa kwa jengo la Westgate na kisha kutekwa kwa raia wa kawaida waliokuwa ndani ya jengo hilo kwa siku nne.
Kwa mujibu wa polisi wa Interpol, mwanamke huyo anasakwa na serikali ya Kenya kwa kumiliki mabomu na kupanga njama ya kufanya mashambulizi kuanzia Disemba mwaka 2011.
Ikiwa mwanamke huyo atakamatwa katika nchi mwanachama wa Interpol, atazuiliwa na kusibiri kupelekwa katika nchi anayotakikana kwa kesi kufunguliwa dhidi yake.
Bi Lewthwaite anajulikana kwa jina bandia la, "Natalie Webb" –na alikuwa anasakwa kwa madai ya kumiliki hati bandia ya usafiri nchini Afrika Kusini.
Ni mjane wa Germaine Lindsay, mmoja wa washambuliaji wanne waliohusika na shambulizi la kigaidi mjini London ambapo watu 52 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa. 
Chanzo: bbcswahili

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 27, 2013

DSC 0064 dad11
DSC 0065 8682d

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...