Friday, May 03, 2013

AGNES MASOGANGE HAISHI KUPIGA PICHA ZA KIMITEGO

SHILOLE......... "BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"

Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa  jina  la   shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila  condom )  ....

Akiongea kwa  kujiamini ,Shilole  alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama  hana  kondom  mkononi.....
Msanii  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kuzilaani   kauli   za  baadhi  ya  watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM"  ladha ya mapenzi inapungua.Yeye  anadai  kuwa  ni  mdau  wa  "GEMU"  hilo  na  huwa  anatumia  NDOM  kama  kawa  na  hufurahia  kama  kawaida...

" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea  mate....Waje  tu , lakini  bila  KINGA wataambulia  PATUPU!!” Alisisitiza Shilole

WOLPER "NAJUTA KUJIINGIZA KWENYE MAPENZI"...!!

DIVA wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper, ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha yake ya huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata hivyo sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua kuyaweka pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa ni mtu wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata mwingine watu hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”

BREAKING NEWZZZZZZZZZZZZZ!!!! : MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 KUSAHISHWA UPYA,

wpid-Prime-Minister-Mizengo-PindaTAARIFA  KUTOKA BUNGENI MUDA HUU AMBAPO WAZIRI LUKUVI  AMETANGAZA KURUDIWA UPYA KUSAHISHWA KWA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE KWA MWAKA 2012,HII IMETOKANA NA MAPENDEKEZO YALIYO TOLEWA NA TUME ILIYO UNDWA KUCHUNGUZA TATIZO LA WANAFUNZI WENGI KUFELI KATIKA HUO MTIHANI,PIA AMESITISHA KUANZA KUTUMIKA KWA VIWANGO VIPYA VYA UFAULU.

MCHUMBA WA MTU ATUPWA JELA KWA KUJIUZA...........!!!


Na Richard Bukos

MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.
Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa
macho.
 
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na kumchukua  kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.
Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.

HII NDIO LIST KAMILI YA VIONGOZI WA TANZANIA NA WA KIMATAIFA WALIOJIUNGA FREEMASONS


Siri ya List za Viongozi wa Tanzania Yatajwa (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.





MWINYI NA ANDY CHANDE


Madai hayo, yametokana na kile kinachoonekana kwamba Kiongozi Mkuu wa Freemason, Afrika Mashariki, Sir Andy Chande, amekuwa akijiweka karibu na viongozi wakuu wa nchi hii kila awamu, hivyo kuonesha kuwa kuna kitu anakitafuta.
Andy Chande

Andy ChandeKikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba kila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri.
Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu na Ikulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi umeonesha kuwa Chande amekuwa karibu na Ikulu tangu Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi mpaka awamu hii ya nne chini
ya Rais Jakaya Kikwete.

NEEMA YAWASHUKIA WALIOFELI .... MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUPANGWA UPYA


TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.

Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.

MAGAZETI YA MAY 3, 2013

.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...