Monday, November 17, 2014

MKAPA ATAKA WAZEE NCHINI WASIBEZWE


Rais Mstaafu Benjamin Mkapa  

Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, amewataka viongozi na Watanzania kutobeza busara na hekima za wazee kwa kuwa bado wana mchango mkubwa kwa Taifa.

Kadhalika mkuu huyo wa zamani wa nchi, alisema kuwa, mzee kuota mvi kichwani haina maana ya kupungukiwa na hekima na maarifa kama wengi wanavyofikiria

Mkapa alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati mahafari ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya St Peter Claver iliyoko nje kidogo ya Mji wa Dodoma.

Alisema anashangazwa kuona maeneo mengi wazee wanapuuzwa na kudharauliwa kama vile hawana mchango wowote kwa maendeleo ya jamii. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PROF. MAGHEMBE ASEMA URAIS SIO MASHINDANO YA UREMBO

Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti hili, walipomfanyia mahojiano maalumu ofisini kwake mjini Dodoma, hivi karibuni. 

Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utitiri wa watu wanaotaka kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2015, akisema nafasi hiyo ya juu nchini haifanani na mashindano ya urembo ambayo mtu yeyote anaweza kujaribu.

Mbunge huyo wa Mwanga alisema watu hao wanaojitokeza kuwania urais hawaelezi wanataka kulifanyia nini Taifa na akashauri wasioweza kueleza hoja zao wasichaguliwe kushika nafasi hiyo.

“Urais unahitaji kuwa na sifa, dira na ajenda kwa Taifa,” alisema Profesa Maghembe wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili mjini hapa.

Kauli ya Profesa Maghembe imekuja wakati Taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, 2015, huku chama chake, CCM kikikabiliwa na kazi ngumu ya kumpata mrithi wa Rais Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SHY-ROSE, SPIKA ZZIWA KIKAANGONI TENA


Mbunge Shy-Rose Bhanji.
Bunge la Afrika Mashariki (Eala) limeitishwa tena, zamu hii jijini Nairobi, Kenya ambako litakutana kuanzia leo mchana, huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wabunge 32 linalotaka kung’olewa kwa Spika wa Bunge hilo, Dk Margaret Zziwa na kuwajibishwa kwa mbunge kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji.
Bunge hilo linakutana baada ya kuahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kukosekana kwa mwafaka baina ya wabunge kwa upande mmoja na baadhi ya wabunge na Spika Zziwa kwa upande mwingine lilipokutana Kigali, Rwanda hivi karibuni. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 17, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAZIRI AJIUZULU KUPISHA UCHUNGUZI

 
Miguel Macedo waziri wa mambo ya ndani wa Ureno aliyejiuzulu 
 
Waziri wa mambo ya ndani wa Ureno amejiuzulu kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za rushwa inayohusishwa na utoaji vibali vya mgawo wa makazi.
Miguel Macedo amesema hahusiki na kashfa hiyo lakini anajiuzulu kulinda heshima ya taasisi za serikali.
Polisi wamewakamata watu 11, akiwemo mkuu wa idara ya uhamiaji nchini humo, siku ya Alhamisi.
Ureno inatoa visa za daraja la kwanza kwa wageni wanaotaka kuwekeza nchini humo.
Mnufaika mkuu wa uharakishaji wa vibali ni raia wa China ambao wamekuwa wakiwekeza kiasi kikubwa nchini Ureno.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAFUA YA NDEGE YATHIBITISHWA UINGEREZA

Ndege wanaofugwa wanakabiliwa na milipuko ya mafua ya ndege

Mlipuko wa mafua ya ndege umethibitishwa katika shamba moja la kuzalishia bata mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa.
Wizara ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini (Defra) imesema hatari kwa afya ya umma ni ndogo sana. Ndege wasiohitajika wanaondolewa kutoka eneo hilo na eneo la kuwatenga limeandaliwa.
Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa Defra.
Kirusi hicho husambaa kati ya ndege na katika matukio ya nadra, kinaweza kuwaathiri binadamu.
Picha ikimwonyesha mchuzi akiuza bata wake katika mtaa mmoja mjini Shanghai,China
Eneo la kuwatenga ndege lililopo kuzunguka shamba hilo litazuia ndege na kinyesi cha ndege ndani au nje ya eneo hilo.Ndege wote pia watatengwa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...