Monday, November 17, 2014

MAFUA YA NDEGE YATHIBITISHWA UINGEREZA

Ndege wanaofugwa wanakabiliwa na milipuko ya mafua ya ndege

Mlipuko wa mafua ya ndege umethibitishwa katika shamba moja la kuzalishia bata mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa.
Wizara ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini (Defra) imesema hatari kwa afya ya umma ni ndogo sana. Ndege wasiohitajika wanaondolewa kutoka eneo hilo na eneo la kuwatenga limeandaliwa.
Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa Defra.
Kirusi hicho husambaa kati ya ndege na katika matukio ya nadra, kinaweza kuwaathiri binadamu.
Picha ikimwonyesha mchuzi akiuza bata wake katika mtaa mmoja mjini Shanghai,China
Eneo la kuwatenga ndege lililopo kuzunguka shamba hilo litazuia ndege na kinyesi cha ndege ndani au nje ya eneo hilo.Ndege wote pia watatengwa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Mlipuko wa ugonjwa hatari wa mafua ya ndege uligundulika Jumapili katika shamba moja nchini Uholanzi.
Tukio hili huko Yorkshire ni la kwanza nchini Uingereza tangu mwaka 2008, wakati ulipozuka. Mafua ya ndege daima yamekuwa yakidhibitiwa kikamilifu nchini Uingereza.

Msemaji wa wizara amesema: "tumethibitisha tukio la mafua ya ndege katika shamba la kuzalishia bata huko Yorkshire - afya za watu haziko katika hatari na hakuna hatari katika vyakula. "Tunachukua hatua za dharura katika kukabiliana na janga hili ambazo zinahusisha eneo la kilomita 10 na kuwaondoa ndege wote katika shamba kuzuia uwezekano wa kusambaa kwa mambukizi. Uchunguzi wa kina kuhusu ugonjwa huo unaendelea.

Tuna rekodi nzuri ya udhibiti na utokomezaji wa milipuko ya ugonjwa wa ndege iliyowahi kutokea siku za nyuma nchini Uingereza." Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...