Monday, May 18, 2015

NKURUNZIZA AWAFUKUZA KAZI MAWAZIRI WATATU

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza .

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita. 

Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara. 

Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.

IS WAUTEKA MJI WA RAMADI


Wapiganaji wa Islamic State

Baada ya mapigano makali kwa siku kadhaa katika mji wa Ramadi nchini Iraq, hatimaye mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa kundi la IS.

Makundi ya wanajeshi wa serikali wamekimbia kutoka katika eneo hilo na Islamic State wamejitangazia ushindi dhidi ya mji huo na kwamba wanaushikilia. 

Mapema msemaji wa Gavana wa jimbo hilo amesema kuwa wapiganaji hao wanayashikilia baadhi ya majengo mhimu ya serikali katika jimbo hilo. 

Hata hivyo umoja wa Mataifa umelaani hatua hiyo ya IS, ambapo pia Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kwa kushirikiana na majeshi ya Shia ili kukabiliana na wapiganaji hao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAN CITY YAICHAPA SWANSEA 4-2

Yaya Toure mshambuliaji wa Man City

Matokeo ya Mechi mbili za ligi kuu ya England zilizochezwa hapo jana,Manchester City iliwachabanga Swansea mabao 4-2 .

Ni Wilfried Bony ambaye mnamo dakika ya 90 lililopigilia msumali wa moto kwa Swansea baada ya kufunga bao la nne.

Lakini Yaya Toure yeye alizifumania nyavu mara mbili dakika 21 na 74. , James Milner naye akifunga mnamo dakika ya 36.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Huku katika mechi ya pili Arsenal wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Man united,ambapo kwa matokeo hayo sasa Arsenal wanaendelea kujiimarisha katika nafasi ya tatu. Leo West Brom watakipiga na Chelsea katika dimba la The Hawthons.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...