Monday, November 04, 2013

GLOBAL EDUCATION LINK YAZINDUA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NJE YA NCHI

Mkurugenzi wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa. Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu.  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE NAYE ANAFUATILIWA NA MAREKANI?

kikwete_2e5c8.jpg
NA MWANDISHI WETU
HATUA ya Marekani kudaiwa kufuatilia mawasiliano ya viongozi wa nchi washirika wake wa karibu, sasa ni wazi imeiacha Tanzania katika wingu la shaka, kama viongozi wake nao wanafuatiliwa kwa namna ile ile inayoelezwa na viongozi wa Ulaya. Shaka hiyo inatokana na urafiki wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Marekani, ambapo kwa nyakati tofauti, marais watatu wa taifa hilo kubwa duniani wamepata kuzuru nchini.
Kauli tofauti zilizotolewa ndani ya wiki hii na majasusi wa mataifa makubwa duniani, ikiwemo Marekani na Uingereza, wakati wakizungumzia madai ya Marekani kufuatilia mawasiliano ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, kwamba nchi zote duniani zinachunguzana, ndiyo ambayo baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanadai kuwa Tanzania bila shaka haiwezi kukwepa kufuatiliwa.


Mbali na hiyo, kauli ambayo imepata kutolewa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la NSA, Edward Snowden, kwamba ujasusi huo wa Marekani haufanywi dhidi ya watuhumiwa wa ujasusi na wakazi wa nchi zenye ugomvi na Marekani tu, bali hata marafiki na waitifaki wa karibu kabisa na nchi hiyo, ndiyo ambayo inajenga mazingira ya Tanzania nayo kuwemo kwenye orodha hiyo ya kufuatiliwa.
Marais watatu wa Marekani, kwa nyakati tofauti wamepata kuzuru nchini. Maraisi hao ni pamoja na Bill Clinton, George W. Bush na Barack Obama, ambaye alitembelea nchini mwezi Julai, mwaka huu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 04, 2013

DSC 0002 de89d
DSC 0003 ae6e5
DSC 0004 db5d9

BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA SIMBA SC

Bobby_3286b.jpg

Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
SIMBA itaanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, Januari 26 mwakani dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa na kocha mpya, Mwanaspoti linaweza kuthibitisha.
Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
Williamson (52), ni straika wa zamani wa West Bromwich Albion na katika mechi 53 aliyoichezea timu hiyo alifunga mabao 11.
Williamson, ambaye ni raia wa Scotland alijiunga na Gor Mahia msimu huu na tayari ameipa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya ikiwa ni miaka 18 tangu timu hiyo itwae ubingwa wa Kenya mwaka 1995.

WAPINGA KUAHIRISHWA KESI YA KENYATTA

130409101249-kenyas-president-elect-uhuru-kenyatta-story-top_ec903.jpg
Waathirika wa kesi inayomkabili rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika, Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana haki kwa waathirika. 
Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...