Saturday, April 18, 2015

WATU 38 WAFARIKI KATIKA AJALI

 Basi dogo aina ya Hiace likiwa limetumbukia kwenye Mto Kiwira eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Ndege, wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Msiba mwingine mzito umelikumba taifa baada ya watu 38 kupoteza maisha katika matukio mawili tofauti, likiwamo la ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace iliyoua watu 19 wakati ikifanya safari ya wizi mkoani Mbeya.

Tukio jingine limetokea mkoani Shinyanga ambako wachimbaji wadogo 19 wa dhahabu waliokuwa katika mgodi mdogo wa Kalole, wilayani Kahama wamekufa baada ya kufunikwa na kifusi usiku wa kuamkia jana kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

 Polisi wakiwa katika machimbo ya dhahabu ya Kalole wilayani Kahama jana baada ya machimbo hayo kuporomoka na kuua watu 19.

Matukio hayo ni mwendelezo wa majanga ya ajali ambazo zimekuwa zikitokea kwa takriban wiki mbili mfululizo na kuua mamia ya watu. Zaidi ya watu 980 wamefariki dunia katika ajali za barabara katika muda wa zaidi ya miezi mitatu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MENGI ATUHUMIWA KWA UHAINI, MWENYEWE AIBUKA NA KUNENA...!!!


MWENYEKITI wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, ametuhumiwa kutaka kuiangusha Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza uongozi wake Oktoba, mwaka huu.

Baada ya tuhuma hizo kuelekezwa kwake na gazeti la Taifa Imara lililochapishwa Machi 23, mwaka huu likiwa na kichwa cha habari kinachosema, ‘Zitto amchongea Mengi kwa JK? Mwenyewe ameibuka Dar es Salaam jana na kuzikanusha mbele ya waandishi wa habari akisema zimemshtua na kumuogopesha.

“Tuhuma zilizotolewa na gazeti la Taifa Imara la Machi 23-29, mwaka huu kwamba nina nia ya kutaka kuiangusha Serikali ya Rais Kikwete na kumshughulikia baada ya kumaliza muda wake wa uongozi, zimenishtua sana,” alisema Mengi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 18, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01472
DSC01469
DSC01470
DSC01471 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

GWAJIMA APANDISHWA KIZIMBANI

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (45), akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

HATIMAYE Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (45), amepanda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka mawili, ikiwemo la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine ni Askofu msaidizi wa Kanisa hilo, Yekonia Behagaze (39), Geofrey Mzava (31) ambaye hakuwepo mahakamani hapo na George Milulu (43) mkazi wa Kimara Baruti.


Kesi hiyo ambayo ilianza kutajwa saa 9:30 alasiri hadi saa 11 jioni, ilisikilizwa mbele ya Hakimu Wilfred Dyansobera, ambapo mawakili wa Serikali; Wakili Mwandamizi Joseph Maugo, akisaidiwa na Shadrack Kimaro na Tumaini Kweka, walisoma mashitaka dhidi ya washitakiwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WASHUKIWA WA UGAIDI WAKAMATWA AUSTRALIA

Mshukiwa wa ugaidi nchini Australia
Polisi katika jimbo la Victoria nchini Australia wanasema kuwa wamewakamata wanaume watano kufuatia oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi kwenye mji wa Melbourne.
Wawili kati ya wanaume hao walio na umri wa miaka 18 walikamatwa baada ya kushukiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi yaikiwemo ya kuwalenga polisi.

Mshukiwa mwingine naye alikamatwa kufuatia sababu zinazohusiana na silaha. Shughuli za kuwatafuta washukiwa wengine zinaendelea sehemu zingine za mji wa Melbourne. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WATU ZAIDI YA 30 WAUAWA AFGHANIISTAN

Eneo kulikotokea shambulizi
Shambulizi la kujitoa mhanga kwenye mji ulio mashariki mwa Afghanistan wa Jalalabad limewaua watu 33 na kuwajeruhiwa karibu wengine 100.

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea karibu na benki ambapo wafanyikazi wa serikali wanalipwa misharaha yao.

Maafisa wanasema kuwa mtu aliyeendesha shambulizi hilo alikuwa na pikipiki.
Kulitokea shambulizi la pili karibu na madhabahu mjini Jalalabad lakini haijulikani kama kulikuwa na madhara yoyote.

Hakuna kundi lililokiri kuhusika, lakini mji wa Jalalabad umekuwa ukilengwa kila mara na kundi la Taliban. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Hii ni kabla ya Mechi za leo Aprili 18, Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.


Rnk
Team MP W D L GF GA +/- Pts

1
Young Africans 21 14 4 3 39 12 27 46

2
Azam 21 10 9 2 27 14 13 39

3
Simba SC 21 9 8 4 27 15 12 35

4
Kagera Sugar 22 8 7 7 21 20 1 31

5
Mgambo JKT 21 8 4 9 17 19 -2 28

6
Stand United 22 7 7 8 19 24 -5 28

7
Mtibwa Sugar 22 6 9 7 21 22 -1 27

8
Coastal Union 23 6 9 8 16 23 -7 27

9
Ruvu Shooting 22 6 8 8 14 20 -6 26

10
Mbeya City 22 5 10 7 17 21 -4 25

11
Ndanda 22 6 7 9 18 24 -6 25

12
JKT Ruvu 23 6 7 10 17 23 -6 25

13
Tanzania Prisons 22 3 12 7 14 21 -7 21

14
Polisi Morogoro 22 4 9 9 13 22 -9 21

ETOILE WAPIGWE TU...!!!

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao katika moja ya mechi katika uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli katika moja ya mechi walizocheza Uwanja wa Taifa.
 
WAPIGWE tu hao Etoile Sportive du Sahel. Ndio kauli ambayo wapenzi wa Yanga na wa mpira wa miguu Tanzania wanaitoa kuelekea pambano la leo la Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga, moja ya timu kongwe nchini, inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuikabili Etoile Sportive du Sahel (ESS) ya Tunisia katika mechi ya raundi ya pili ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Vijana hao wa Jangwani ndio timu pekee iliyobaki ya Tanzania katika michuano ya kimataifa na ndio maana wapenzi wake, mashabiki wa soka nchini na Watanzania kwa ujumla, wangependa kuiona inaipiga ESS na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika marudiano Mei Mosi, mwaka huu, mjini Sousse. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KOCHA ETOILE AINGIA MITINI...!!!

faouzibenzarti
Kocha Mkuu wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Faouzi Benzarti

KOCHA Mkuu wa Etoile du Sahel ya Tunisia, Faouzi Benzarti, ameingia mitini baada ya kushindwa kutokea katika mkutano wa makocha na waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Benzarti alishindwa kuhudhuria mkutano huo kwa madai walichoka baada ya kuwa angani kwa saa tisa wakitokea Tunisia ambapo waliwasili Dar es Salaam jana alfajiri.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, Benzarti aliwataarifu kwamba asingefika kwenye mkutano huo na kuwaomba radhi kutokana na hilo.

Pamoja na kushindwa kutokea kwa kocha huyo, Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm alisema amezikamata mbinu za Etoile du Sahel na atahakikisha wanashinda mchezo huo wa raundi ya pili wa Kombe la Shirikisho Afrika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...