Friday, April 19, 2013

BABA KANUMBA HAONI ULAZIMA WA KULIONA KABURI LA MWANAE KANUMBA

BABA wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba amefunguka kuwa haoni ulazima wa kuliona kaburi la mwanaye na kuhusu kufanya maombi mwaka mmoja baada ya kifo, alifanya akiwa huko nyumbani kwake Shinyanga.
Akizungumza kwa njia ya simu hivi karibuni, mzee Charles alisema mtu anapofariki kikubwa ni kuombewa na hilo la kwenda kulitazama kaburi lake haliwezi kuwa na faida.
“Mimi nilifanya sala ya kumuombea Kanumba pamoja na mtoto wa dada yake ambaye walikufa kwa kufuatana kwenye Kanisa la AIC Shinyanga,” alisema mzee huyo na kuongeza;
“Mtu akishakufa kinachobaki ni kumuombea huko aliko na kaa ukijua kwamba huku ndiyo kwenye chimbuko la marehemu hivyo nisingeweza kwenda kufanyia maombi kwenye mji mwingine.”

'Chadema kuwa na mabalozi nyumba 10'

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbrod Slaa
--
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kimeanza mkakati kuhakikisha kinakuwa na mabalozi wa nyumba kumi kwa kila eneo. Hatua hiyo ni katika kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi kitongoji .
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Wilbrod Slaa alisema hatua hiyo imeanza kwa kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya taifa ya chama hicho.

Alikuwa akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa taifa waweze kwenda kutoa mafunzo ngazi ya kanda ambao nao wataendelea kutoa elimu hiyo kwenye jimbo kata hadi vijiji.

Lengo la chama hicho ni kuhakikisha kinajiimarisha na kuwa na viongozi wenye kufuata maadili na misingi ya chama na kujiandaa kushika dola kwa kuwa na uongozi wenye weledi wa hali ya juu, alisema. 


“Sisi hatutaki mwanachama anunue shashada ya kura, tunajiandaa tunapeleka silaha ya kujiandaa kushika dola na ndiyo maana tunawaandaa kuhakikisha tunaposhika dola, tunakuwa tayari na viongozi wenye weledi mkubwa,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa aliwashangaa watu wanaodai kuwa M4C imekufa.

Alisema watu hao hawajui kuwa Chadema imejipanga na ina mbinu za utawala ambazo hazina hila kama baadhi ya vyama vingine vinavyofanya.

“ Navishangaa vyama vingine vinasifika kwa hila badala ya kuijenga Tanzania na wananchi wake… serikali za mitaa hadi wilaya ni wizi mtupu sisi tunatengeneza wataalamu wenye uchungu wa kulinda rasilimali zao,” alisema.
Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa chama hicho, Benson Kigaula alisema inategemewa watafundishwa wakufunzi 30,606 ambao watavifikia vitongoji vyote nchini.

Alisema hadi Oktoba mwaka huu vijiji 18,000 vitakuwa vimefikiwa na kupewa walimu na wakufunzi hao.

OBAMA ATOA KAULI KUHUSU JAY Z NA BEYONCE KUTEMBELEA CUBA.

Rais wa Marekani Barack Obama ameikana ziara ya rapa nyota nchini humo Jay- Z na mke wake Beyonce akisema kuwa hana habari na safari yao waliyoifanya hivi karibuni kwenda nchini Cuba

Hivi karibuni Jay Z na Beyonce walisafiri kwenda nchini Cuba kwa ajili ya kuadhimisha miaka mitano ya ndoa yao jambo lilolosababisha maofisa wa Chama cha Republican kutaka ufanyike uchunguzi ama amevunja vikwazo vya kusafiri

Akiwa nchini humo rapa huyo alizindua kibao chake alichokipa jina la'Open Letter' ambacho mashahiri yake yanaonekana kama Obama alikuwa amemzuia kufanya ziara hiyo,hata hivyo taarifa iliyotolewa na Msemaji wa White House, Jay Carney ilieleza kuwa utawala wa Serikali ya Rais Obama ulitoa baraka zote kuhusu safari hiyo ya Jay Z kwenda Cuba na kwa sasa rais huyo ametoa kauli kama hiyo

Rais Kikwete amemteua Bw. Raymond Mbilinyi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Raymond P. Mbilinyi(Pichani) kuwa Katibu Mtendaji, Baraza la Biashara la Taifa , (TNBC).

Taarifa iliyotolewa leo, Ijumaa, 19 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Machi 4, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Raymond P. Mbilinyi  alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendanji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na anachukua nafasi iliyoachwa na Bwana Dan Mrutu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
19 Aprili, 2013

RAIS UHURU KENYATTA AMEITANGAZA STRUCTURE YA SERIKALI YAKE

President Uhuru Kenyatta unveils the structure of his Government, In exercise of the authority vested in him by the Constitution of Kenya 2010 and in conformity with the expectations of a lean and effective structure, President Kenyatta officially released the list of ministries and state departments that will form the National Executive as follows:
Under the Presidency, there will the Executive Office of the President and the Executive Office of the Deputy President with two ministries:
Ministry of Interior and Coordination of National Government.
Ministry of Devolution and Planning.

Other ministries are: 3. Defence 4. Foreign Affairs. 5. Education which will have the Department of Education and Department of Science and Technology 6. The National Treasury 7. Health 8. Transport and Infrastructure which will have the Department of Transport Services and the Department of Infrastructure.
9. Environment, Water and Natural Resource 10. Land, Housing and Urban Development 11. Information, Communication and Technology (ICT) 12. Sports, Culture and the Arts 13. Labour, Social Security and Services 14. Energy and Petroleum 15. Agriculture, Livestock and Fisheries under which are the Department of Agriculture, Department of Livestock and Department of Fisheries 16. Industrialization and Enterprise Development.
17. Commerce and Tourism which has the Department of Commerce and Department of Tourism 18. Mining, The structure also contains the Office of the Attorney General and Department of Justice.

In the new structure, President Kenyatta has collapsed the ministries from 44 to 18. The reduced structure is geared towards achieving a lean, efficient and effective executive branch of Government.
In the structure, the President has given special focus to the youth, gender, devolution, planning as well as national cohesion and integration which have all been brought under the Presidency.

Also given special focus is mining which is now a stand-alone ministry. Information, Communication and Technology ministry as well as Sports, Culture and Arts are also stand-alone ministries with a view to leveraging on the creative potential of the youth. Infrastructure ministries as well as national resources ministries have also largely been brought under the same roof. Picha na Millard Ayo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya akionyesha kitabu alichokiandika kwa wabunge wakati akichangia Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Uratibu na Mahusiano kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi. Picha na Pamela Chologola.
Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu),Profesa Mark Mwandosya ametoa majibu kwa wanaoisakama Idara ya Usalama wa Taifa akilieleza Bunge kuwa ni muhimu ikatafutwa kamati itakayokuwa inajadili masuala ya idara hiyo na si bungeni.
Profesa Mwandosya alisema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2013/14.
Juzi wakati wa kuwasilisha hoja kambi rasmi ya upinzani bungeni,iliitaka Serikali kuwachukulia hatua maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa–Ikulu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya utekaji na utesaji watu wanaoonekana kuikosoa Serikali. Madai hayo yalitolewa bungeni na msemaji wa kambi hiyo, kuhusu bajeti ya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Profesa Kulikoyela Kahigi katika hotuba ambayo awali ilizua mvutano wa mambo gani yasomwe na yapi yabakiwe.
Hata hivyo katika kikao hicho hotuba hiyo iliamriwa iahirishwe kwa muda,hadi kamati ya kanuni ikutane na kutoa uamuzi wa baadhi ya mambo yanayotaja majina ya watumishi wa usalama wa taifa na mengine yaliyoko mahakamani yaondolewe.
Akizungumzia hali hiyo, Mwandosya alisema anashangazwa na watu wanaozungumza kuhusu usalama wa taifa kama vile ni ndugu zao au marafiki kitu ambacho si sawa.
“Usalama wa Taifa hauwezi ukawa unazungumzwa tu hivi hivi, inatakiwa kuwe na kamati ya kuujadili kama ilivyo kwa nchi za wenzetu Marekani, Uingereza katika mashirika yao kama FBI na MI6,”alisema Profesa Mwandosya na kuongeza:
“Usalama wa taifa hauwezi ukazungumzwa hapa kuna sehemu ya kuzungumzia kwani kuzungumza hapa ni sawa na kujianika, usalama hauwezi kuwa wa kutoa kucha watu kwani utakuwa huo si usalama bali ni uhalifu.”
Wakati huo huo, Mbunge wa Longido, Michael Laizer amependekeza Bunge la sasa livunjwe ili Serikali itangaze uchaguzi mpya kutokana na wabunge wengi kutojua wajibu wao.
Mbali na hilo, mbunge huyo amevitaka vyama vya siasa vyenye wabunge kukutana na wabunge wao na kujadiliana namna bora ya kulifanya Bunge liwe na heshima mbele ya Watanzania.
“Hapa hakuna mtu anayestahili kuitwa mbunge, maana sioni mwenye heshima hiyo”, alisema Laizer.
Mwananchi

SPIKA MAKINDA AZUNGUMZIA JUU YA UAMUZI WA KUWAFUKUZA WABUNGE ULIOFANYWA NA NAIBU WAKE, NDUGAI

Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo
Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na wengineo, na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge, Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba Muongozo/Taarifa mara kwa mara, Hivyo Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao, na baadae kitendo cha wabunge hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka nje ya Bunge pamoja na kuwagomea Askari wabunge, kitendo ambacho kidogo kizue masumbwi live, Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge, Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliotolewa.
Photo
Taswira ya vurugu zilizotokea bungeni dodoma jana ambapo Mbunge wa mbeya Mh mbilinyi akiskiwa pamoja na wenje, lema na wengineo wakionekana kwa pamoja wakiwazuaia askari ili wasimtoe nje mh Tundu lissu aliyeamriwa na naibu spika atolewe nje ya ukumbi wa bunge

hapa waziri wa nchi na uratibu wa bunge Mh William Lukuvi akiwaeleza jambo wabunge wa chadema mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa baada ya kutokea vurugu bungeni

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA AKIUMBUA CHADEMA

Aliyekuwa Mweyekiti wa Chadema Kata ya Mkalama Gairo Mkoani Morogoro, Zefania Magida akikaboidhio kadi yake kwa Kinana baada ya yeye na wenzake 689 kutangaza kuhamia CCM katika kutano wa hadhara uliofanyika jioni hii kwenye uwanja wa shule ya msingi Gairo B,wilayani Garo mkoani Morogor


Zefania Magiga aliyekuwa Mwenyekiti wa kata Chadema,akitangaza rasmi kuhamia CCM kwenye Mkutano wa hadhara ulifanyika Gairo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana


MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 19.04.2013

3 4c53d
1 4c59c
2 f51a0

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...