BABA
wa marehemu Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba amefunguka kuwa haoni
ulazima wa kuliona kaburi la mwanaye na kuhusu kufanya maombi mwaka
mmoja baada ya kifo, alifanya akiwa huko nyumbani kwake Shinyanga.
Akizungumza
kwa njia ya simu hivi karibuni, mzee Charles alisema mtu anapofariki
kikubwa ni kuombewa na hilo la kwenda kulitazama kaburi lake haliwezi
kuwa na faida.
“Mimi
nilifanya sala ya kumuombea Kanumba pamoja na mtoto wa dada yake ambaye
walikufa kwa kufuatana kwenye Kanisa la AIC Shinyanga,” alisema mzee
huyo na kuongeza;
“Mtu
akishakufa kinachobaki ni kumuombea huko aliko na kaa ukijua kwamba
huku ndiyo kwenye chimbuko la marehemu hivyo nisingeweza kwenda kufanyia
maombi kwenye mji mwingine.”
No comments:
Post a Comment