Saturday, May 04, 2013

SAKATA LA PADRI ALIYENASWA NA MKE WA MTU..... MAPYA YAIBUKA BAADA YA MUME KULIPONDA KANISA KATOLIKI....!!


 

LILE saga la madai ya fumanizi la Padri Urbanus Ngowi aliyekuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishiwa Makomu, Marangu limeibua mtikisiko mkubwa kwa Kanisa Katoliki nchini, .
KWANI ILIKUWAJE?
Katika habari iliyofichuliwa , Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P.

 
Mara baada ya ‘mzigo’ huo kuingia mitaani nchi nzima, mhariri wa gazeti hilo (jina linahifadhiwa) alianza kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kona mbalimbali kwa watu waliojitambulisha kuwa ni waumini wa kanisa hilo wakidai kushtushwa na tukio hilo.

VIKAO VIZITO
Habari za ndani kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi zilieleza kuwa baada ya ishu kuwa ‘hoti’, viongozi wa jimboni hapo, Jumatatu iliyopita walikaa vikao vizito kulijadili suala hilo na kulitolea uamuzi.
Ilidaiwa kuwa uongozi ulikubaliana kumwita mume wa Mama P ambaye wakati tukio hilo likitokea alikuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi.
Ilisemekana kuwa waliwasiliana na mwanaume huyo ambaye alitakiwa kuondoka Dar, Alhamisi iliyopita kwenda Moshi kukutana na viongozi hao kwa lengo la kuweka mambo sawa.
Ilidaiwa kuwa jamaa huyo ambaye amezaa na Mama P watoto wawili, alikubali kukutana na viongozi hao kwa shingo upande huku akitishia kulipeleka suala hilo mbele zaidi kwa kuwa alishalalamika muda mrefu kwamba Father Ngowi ana ukaribu wenye maswali mengi na mkewe.Tulitonywa kuwa baada ya mwenye mke huyo kulalama sana, Father Ngowi aliitwa na uongozi wa jimbo hilo kisha akaonywa lakini hakuna kilichobadilika.

PENNY...... "SINA MIMBA YA DIAMOND, NAMSHANGA ANAVYOTANGAZA KWA WATU"

HIVI karibuni, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliripotiwa akisema demu wake ambaye ni ‘prizenta’ wa Runinga ya DTV, Peniel Mungilwa ‘Penny’ ana ujauzito wake na kwamba amemnunulia ‘mkoko’ (gari) la mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kwenda nalo kliniki, Penny ameifungukia kauli hiyo.
Akizungumza na mapaparazi wetu kwa njia ya simu jijini Dar juzikati, mrembo huyo alionesha hali ya kupaniki huku aking’aka na kushangazwa na habari hizo za ujauzito.
 
 Alisema amekuwa akisoma habari za ‘mimba’ yake kupitia magazeti lakini hajaulizwa na mwandishi yeyote, jambo linalomshangaza sana.
Alipoambiwa kwamba aliyesema habari kwamba yeye ana mimba ni Diamond, Penny alisema: Namshangaa! Ni mimba ipi kwanza?
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema mbali na madai ya mimba, lakini pia uhusiano wake na msanii huyo unamnyima raha kutokana na maneno ya watu.
Baada ya waandishi kujitambulisha, mahojiano yalikuwa hivi:

Funguka: Vipi, ujauzito unaendeleaje? Ni kweli una mimba ya Diamond au umeshaitoa?
Penny: Mh! Yaani sijui hata niseme nini, nashangazwa sana na hizi habari, nazisikia tu halafu mimi mwenyewe mhusika sijapewa nafasi ya kuzungumza.
Unajua sijazoea maisha haya ya kila wakati kuzungumza na waandishi. Naomba mniache, nani aliwaambia kuwa mimi nina mimba?
Funguka: Diamond.
Penny: Kama ni Diamond muulizeni yeye mwenyewe! Mbona nakosa raha jamani?
Funguka: Vipi mna mpango wa kuoana na Diamond?
Penny: (kwa hasira) Hizo ni ishu zangu binafsi, kama tutaoana au hatuoani ni mipango yetu, sioni sababu ya kutangaza kwenye media.
Funguka: Unaichukuliaje kauli ya mama mkwe wako, yaani mama Diamond? Inadaiwa alisema hatambui uhusiano wowote wa mtoto wake na mwanamke mwingine hadi atakapofunga ndoa.
Penny: Tafadhali sana, sitaki kuzungumzia habari kuhusu mama Diamond. Kwa hilo ‘no comment.’
Funguka: Vipi lakini, unainjoi kuwa na uhusiano na Diamond?
Penny: (Akakata simu).
Funguka: Haloo… haloo!
Hata hivyo mapaparazi wetu walipojaribu kumpigia simu tena hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu mpaka kukatika yenyewe.

Ruge Mutahaba kumjibu Lady Jay Dee Jumatatu


Kwenye kipindi cha Power Breakfast kitakacho rushwa siku ya jumatatu saa mbili asubuhi Ruge Ataongelea issue ya Jay Dee ,Lady Jay Dee ameingia kwenye vita kali na Clouds Fm huku akimshambulia Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kwa madai kuwa ndio wanaokula jasho la wasanii.

MAGAZETI YA MAY 4 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

WABUNGE:: SERIKALI SASA IWANG'OE VIONGOZI NECTA


Baadhi ya wabunge na wadau wa elimu wametaka Serikali kutoishia kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, bali iwajibishe Baraza la Mtihani Tanzania (Necta) kwa kufelisha wanafunzi.

 
Akizungumza kuhusu kauli ya Serikali kufuta matokeo hayo jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza alisema taarifa ya tume ingekuwa tofauti na ilivyotolewa ilikuwa isababishe vurugu nchini.

“Kauli hii ya Serikali ndiyo iliyotegemewa na wadau wa elimu, tume wangefanya vinginevyo tunge-riot (fanya vurugu), kwa sababu matokeo yaliyotolewa na Necta siyohalisi. Tume imefanya kazi nzuri na kilio cha wanafunzi kimesikika,” alisema Rweikiza na kuongeza:

“Sasa na hili nalisema bila kificho, Necta lazima wawajibishwe kwa sababu wanafunzi wanne wamejiua kwa matokeo hayo yasiyo halali, kule kwangu (Bukoba Vijijini) wanafunzi wamekata tamaa na wanaolewa. Hiyo yote ni hasara ambayo haina wa kuilipa.”

Aliongeza kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo Marekani, mtihani wa mwisho hauchukuliwi kama kigezo kwa sababu inategemea mwanafunzi jinsi alivyoamka siku ya mtihani na kwamba, wanatumia mitihani iliyopita kufanya tathmini yao.

IZZO B......... "SINA MAHUSIANO NA WEMA WEMA SEPETU"

Siku chache baada ya kukwenda Arusha kwa mapumziko mafupi kutokana na kudhalilishwa na mpenzi wake wa dhamani Diamond kupitia redio...Beutifully onyinye wa Bongo, sasa hausishwa kutoka kimapenzi na msanii wa hip hop Izzo bizness..
  izzo bizness kupitia xxl ya clous fm chini ya u-heard ya alhamisi ya wiki hii alikanusha kabisa kuwa na mahusiano ya mrembo wema na kuthibitisha kuwa wao ni washikaji na wanakutana mara mojamoja ingawa wenyewe wamezoea kuitana 'darling' kwa mazoea..
KuSikiliza  kauli ya izzo bizness bfya hapo chini !!

GADNER....... "KAMA ASINGEKUWEPO LADY JAYDEE BASI NINGEKUWA NA VANESSA MDEE"

MUME wa Legend wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jadee’, Gardner G Habash ‘Kapteini’ aliwaacha watu midomo wazi baada ya kusema kama angekuwa hajaoa, basi angemuoa msanii anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Vanessa Mdee.
Kapteini alitamka hayo juzi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 kilichochukua nafasi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mume huyo wa Lady Jaydee alikuwa MC wa shughuli hiyo hivyo kutumia kipaza sauti kumnadi Vanesa.
Gardner G Habash ‘Kapteini’.
“Kiukweli Vanesa ni msanii mzuri, ana uwezo mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop na kulitawala jukwaa. Ningekuwa sijaoa kwa kweli ningemuoa Vanesa Mdee,” alisema Gardner.
Mbali na Vanesa, wasanii wengine wanaounda familia ya B Heatz walipata nafasi ya kutumbuiza katika hafla hiyo akiwemo mkongwe, Ally Baucha

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...