Sunday, November 16, 2014

MTOTO ANAYEDAIWA KUGEUKA NYOKA AZUA KIZAA ZAA

Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi minne amezua kizaazaa cha aina yake, baada ya kuwapo taarifa kwamba mara kadhaa umbo lake limekuwa likigeuka na kuwa nyoka na mwili wake ukiendelea kudhoofu kutokana na kukataa kunyonya maziwa ya mama yake.
Mtoto huyo (jina lake tunalihifadhi kwa sasa), wiki iliyopita alivuta umati wa wakazi wa Kijiji cha Nkome mkoani Geita ambao walifurika ndani na nje ya Kanisa la AICT Nkome, lililopo kijiji hapo, kushuhudia maombi ambayo alikuwa akifanyiwa ili kumkomboa katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni mateso dhidi yake.
Ilikuwa saa 4.00 asubuhi Jumamosi, Novemba 8 mwaka huu wakati mtoto huyo alipofikishwa katika kanisa hilo na kuanza kufanyiwa maombi na sababu ya hatua hiyo ikielezwa kuwa ni kutokana na kuwa na umbo la nyoka na kwamba matendo yake yanaashiria kwamba mwenye asili ya nyoka ndani ya roho yake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE AILIPUA SERIKALI KUHUSU BANDARI BUBU NCHINI

 
Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. PICHA|MAKATBA  

Mwenyekiti wa Chacha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuwa uwepo wa bandari bubu zinazopitisha bidhaa kwa magendo kutoka nje ni miongoni mwa sababu zinazoua viwanda vya sukari hapa nchini.
Amesema kuwa viwanda vya miwa vinapokufa, wanaoumia siyo wenye viwanda bali wakulima wa miwa. Mbowe alisema hayo juzi alipohutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho mjini Turiani , Mkoa wa Morogoro katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.

Ziara hiyo ni ya Operesheni Delete CCM (ODC) yenye lengo la kuvihamasisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuiondoa CCM madarakani kuanzia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PINDA AHIMIZA KUCHANGIA ELIMU

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. PICHA|MAKTABA 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu, badala ya kujikita kuchangia sherehe za harusi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kwebwe aliyezungumza kwa niaba ya Pinda katika sherehe ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anuarite iliyopo Makoka, jijini Dar es Salaam.
“Urithi pekee kwa watoto wetu ni elimu, unaweza kumwachia mali, lakini itakwisha, ukimwachia elimu hakika huu ndiyo urithi pekee…: Watanzania wenzangu, tujitoe kuchangia sekta ya elimu kama ambavyo tunafanya katika sherehe,” alisema Kebwe akiongeza:
“Utamkuta mtu anachangia fedha nyingi katika harusi na kama tunavyojua harusi moja, ukianza na ‘send off’, ‘kitchen part’ na harusi yenyewe ni fedha nyingi, lakini mtu huyo huyo ukimwambia achangie masuala ya elimu, hutamwona.”
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Gaudence-Makoka wamiliki wa shule hiyo, Padre Evarist Tarimo, alisema kuwa malengo ya sherehe hiyo ni kuchangisha Sh250 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa bweni la wavulana ili kuondoa adha wanayoipata kwa sasa.
“Hivi sasa vyumba vya madarasa tunavitumia kama mabweni, hivyo wanasomea humo na kulala humo humo, jambo ambalo kitaaluma si zuri. Tunatarajia tutakapomaliza ujenzi huo tutawawezesha wanafunzi wetu kusoma na kulala katika mazingira mazuri na nina hakika juhudi za wadau zitaweza kukamilisha ujenzi huu,” alisema. Habari tulizozipata baadaye zilisema jumla ya Sh41.2 milioni zilikusanywa. Fedha taslimu ni Sh13.3 milioni. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 16, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
. 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...