Thursday, April 30, 2015

MWANAFUNZI AUAWA BAADA YA KUKUTWA NA BARUA YA MAPENZI

        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda

MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15) anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35) baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na rafiki wake wa kike.

Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Majengo ‘D’ Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi huyo, ambaye ni mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa zaidi ya saa tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha tukio hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita. Alisema bado wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya kitendo hicho alitokomea. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SARAFU YA SH. 500 YATENGENEZEWA MIKUFU

miatano
Sarafu mpya ya shilingi 500


SARAFU mpya ya shilingi 500 inadaiwa kuhujumiwa na baadhi ya watu ambao huinunua kwa Sh 2,500 na baadaye kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha (silver).

Taarifa ambazo MTANZANIA imezipata kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza tangu sarafu hizo zilipotolewa kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka jana, baadhi ya watu wamekuwa wakizikusanya na kuzifanya kuadimika mtaani.


Imeelezwa kuwa tangu kutolewa kwa sarafu hiyo imekuwa adimu mitaani jambo ambalo si kawaida kwa fedha mpya zinazoingizwa kwenye mzunguko kuadimika kwa kiwango hicho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'TUTAWAREJESHEA WANANCHI MAJIMBO TATA' DL SLAA

http://jambotz8.blogspot.com/
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Slaa

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema endapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vitashindwa kuafikiana katika kuachiana baadhi ya majimbo kabla ya Uchaguzi Mkuu, watawaeleza wananchi kwa kuwa ndiyo kiini cha kuanzishwa kwa umoja huo.

Dk Slaa alisema hayo jana kabla ya kumalizika kwa vikao vya wakuu wa Ukawa ambao wamekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia ngazi ya urais, ubunge na udiwani na kwa siku mbili kuanzia juzi, walikuwa wakijadili ufanikishwaji wa azimio hilo.
Dk Slaa alisema hadi sasa wameshakubaliana kuachiana asilimia 95 ya majimbo yote na kwamba ana matumaini watafanikisha, lakini akaonya kuwa ikishindikana, hawatasita kuwaeleza wananchi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ALI KIBA, DIAMOND, JUX WAPETA TUZO ZA KILI

alikiba1
Ali Kiba


WASANII wa muziki wa bongo fleva, Ali Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Juma Jux, wameingia katika vinyang’anyiro sita vinavyogombewa katika tuzo za muziki ‘Kili Music Award’.
Ali Kiba ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora wa muziki wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume, mtunzi bora, video bora ya mwaka na mwimbaji bora wa Afro-Pop.

jux
Juma Jux

 
Naye Diamond ameingia kwenye kipengele cha mtumbuizaji bora, mwimbaji bora, mtunzi bora, wimbo bora wa Zouk, wimbo bora wa Afro Pop na Video Bora ya mwaka kupitia wimbo wa ‘Nitampata Wapi’ na ‘Mdogo Mdogo’.
Diamond
Nasibu Abdul ‘Diamond’

Pia Juma Jux naye ameingia kwenye kipengele cha mwimbaji bora wa kiume, wimbo bora wa mwaka, mtunzi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kiume na wimbo bora wa R&B kupitia nyimbo zake mbili za ‘Sisikii’ na ‘Nitasubiri’.


Mkuu wa matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania Basata, Kurwijira Maregesi, alisema zoezi rasmi la upigwaji wa kura litaanza Mei 4 na kufungwa Juni 5 mwaka huu kwa udhamini mkubwa wa Kampuni ya TBL, kupitia bia yake ya Kilimanjaro. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

'SITAVAA NGUO ZA UTUPU TENA' SNURA MAJANGA

snura
Snura Mushi ‘Majanga’


MWIGIZAJI na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Majanga’, amesema hatavaa tena nguo za nusu uchi kwa kuwa ameshagundua makosa hayo.

Snura alisema awali alikuwa akivaa mavazi ya nusu uchi au nguo za kumbana, lakini kwa sasa amejirekebisha na anatambua nguo zinazompendeza ili kutokuleta sintofahamu kwa mashabiki wake.


“Kiukweli nashukuru ushauri wa watu katika suala la mavazi, nimeshajirekebisha kwa sasa sivai kama zamani mavazi yasiyofaa katika jamii,” alieleza Snura. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UGAIDI GARISSA, VYOMBO VYA USALAMA VILIZEMBEA

Watu 150 walipoteza maisha kwenye shambulio la Garissa
Waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Generali Joseph Nkaiserry amekiri kwamba vyanzo na duru za kijasusi zilitahadharisha lakini zilipuuzwa kabla ya shambulizi la Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garrissa.

Karibu watu 150 walikufa wakati wa shambulio hilo. Waziri Nkaissery ameongeza kusema shughuli za wokozi zilizofuata pia zilifanywa kiholela.

Baadhi ya Maafisa wakuu wa polisi wamesimamishwa kazi kufuatia shambulia hilo la Chuo Kikuu cha Garrissa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC Swahili

KIJANA MDOGO AOKOLEWA AKIWA HAI SIKU BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI...!!!

Kijana aokolewa siku tano baada ya kufunikwa na kifusi
Watoa huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi kukumba taifa hilo siku tano zilizopita.

Licha ya kuwa chini ya maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.

Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo. Wengi wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa miundo mbinu.

Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...