Sunday, June 02, 2013

DIAMOND ATOA SIRI YAKE NA MANGWAIR.

 
DIAMOND.

 https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTcbPsmB8oL0NdNY9ZTMuOtFcF-881836OfLxvYzL9xEVxaoG1Z5Q


WAKATI watu mbalimbali maarufu nchini, hususan wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), wakiendelea kutoa historia ya mahusiano yao na aliyekuwa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mangweair.

wea, msanii maarufu wa muziki nchini Nassib Abdul (Diamond Platnumz) amevunja ukimya na kutoa siri yake na marehemu Mangwea.

Akielezea hisia zake pamoja na mipango mingi aliyokuwa nayo kuhusu kufanya kazi ya muziki na marehemu katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond alisema kwamba alijaribu kufanya kazi ya pamoja na msanii huyo lakini kwa bahati mbaya kazi zote zikaharibika.


"Kinacho niumiza ni jinsi tulivyo jaribu kutengeneza HIT bila mafanikio yaani siyo nilizo mshirikisha hata zile alizo nishirikisha na tuka amua kuplan kutengeneza nyingine akirudi kutoka Afrika Kusini, lakini haikuwezekana yani mungu alimpenda zaidi":alisema Platnumz.


Kila binadamu huwa na jambo lake muhimu ama siri ya mafanikio baina yake na mtu mwingine ambayo pengine si rahisi kuizungumzia hadharani ama wakati wowote, lakini inapotokea mmoja kati yao akifariki dunia anayebaki duniani hujikuta akitoa siri hiyo.


Hatua ya Binadamu kuamua kutoa siri yake na mwenzake wakati wa msiba wa mmoja wao inaweza ikawa na tafsiri nyingi lakini ukweli nikwamba huzuni na machungu ya kuondokewa na mtu muhimu kwake aliyekuwa akitarajia kufanya naye jambo flani muhimu ndiyo husababisha mtu huyo kutoa siri.R.I.P Mgwea.

DEREVA MWANAMKE WA BASI LA NDENJELA COACH AWA KIVUTIO KWA ABIRIA

DEREVA NUSURA MAGULUKO 28 AKIMWOMBA MUNGU KABLA YA KUANZA SAFARI
SASA HAPA YUPO KAZINI
BAADHI YA ABIRIA WAKIFURAHIA MWENDO MZURI WA DEREVA NUSURA MGULUKO

ABIRIA WAKIPATIWA HUDUMA YA VITAFUNWA NDANI YA BASI HILO LA NDENJELA

MISS SHINYANGA CENTRE APIGWA NA KUNYANG'ANYWA PESA NA MUANDAAJI WA SHINDANO HILO BAADA YA KUKATAA KUONDOKA NAE....!!!

 



Na Mwandishi wetu Steve Kanyeph
Mashindano ya kumtafuta mrembo Shinyanga yaani Miss Shinyanga Centre yamemalizika huku yakiingiwa dosari baada ya mshindi wa taji hilo SCOLASTIKA SITTA{19} kutoa malalamiko kuwa amedhalilishwa kwa kupigwa na kunywanganywa pesa kiasi cha shilingi laki 3 alizopewa ikiwa ni zawadi
mrembo huyo amesema tukio hilo limefanywa na muuandaaji wa mashindano ya miss Shinyanga ASELA MAGAKA baada ya mrembo huyo kukataa kuondoka kwenda Kahama usiku wa manane.

“Alitaka tuondoke baada ya kushuka jukwaani na twende Kahama kwaajiri ya kambi ya miss Shinynga usiku huo huo mimi nikakataa kwa sababu ilikuwa ni usiku sana na baada ya hapo akapanick akanipiga makofi na kuninyang'anya pesa zote shilingi laki 3”.Alisema mrembo huyo.




Mrembo huyo amesema kitendo hicho ni cha udhalilishaji na kimemkatisha tamaa ya kuendelea kushiriki mashindano kwa ngazi ya mkoa na amekwenda kutoa taarifa polisi na taratibu za kisheria zinaendelea.
Scolastica anatoa ushauri kwa waandaaji wa mashindano ya urembo kutowadhalilisha washiriki na kwamba warembo wanatakiwa kuwa imara na jasiri katika kudai haki zao na kupinga vitendo vya udhalilishaji kwani mashindano ya urembo yanakabiliwa na changamoto nyingi.

WANYARWANDA WANASWA WAKIJIUZA JIJINI DAR


POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.


Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.

Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.


“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?

Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.

Waliosomewa mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru  Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo 35.
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

WAZIRI MKUU ACHARUKA KASI NDOGO YA UJENZI WA BARABARA RUKWA

20120913_164754
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 *Afanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya wajenzi wa Kichina
*Aahidi kumtuma Waziri Magufuli kufuatilia, ataka mkandarasi aongeze kasi, awe makini
*Amtaka RC Rukwa aunde timu ya kumpatia ripoti kila mwezi
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda jana jioni (Jumamosi, Juni Mosi, 2013) alilazimika kufanya ziara ya ghafla kwenye kambi ya wajenzi wa barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni ili kupata maelezo ni kwa nini kazi hiyo inasusua na haionyeshi kuendelea.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa akitoka Namanyere, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Rukwaalilazimika kusimama kwenye kambi hiyo ya wajenzi iliyopo Paramawe, wilayani Nkasi.

Wasemavyo wasanii kuhusiana na kifo cha Ngwea

Kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea ambaye amefariki nchini Afrika ya Kusini ambako alikwenda kufanya maonyesho, wasanii mbalimbali  wamezungumzia kifo chake.
Ni dhahiri, Albert Mangwea alikuwa katika kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi na ndiyo uhai wake ulikopotea, Mwandishi wetu Kalunde Jamal aliongea na baadhi ya wasanii wenzake na maongezi yakawa kama ifuatavyo:
Joseph Haule a.k.a Profesa Jay
Anasema katika hili hakuna jinsi kwa kuwa kila binadamu atayaonja mauti.
“Inaniuma sana lakini sina cha kufanya kwa kuwa ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa, kinachotakiwa ni kumuombea apumzike kwa amani  huko aendako.         
Selamani Msindi ‘Afande Sele’
Anasema anamtambua Ngwea siyo kama msanii bali ni mdogo wake wa karibu na ameshindwa kujizuia kutoa machozi kuhusiana na kifo hicho.
Anaongeza kuwa katika kuonyesha ni kwa jinsi gani kijana huyo alikuwa na mapenzi na watu kwani kwao ni Morogoro lakini alijulikana ni kijana wa Dodoma almaarufu East Zoo.
Ngwea kapambana na muziki ukiwa hauna mbele wala nyuma kapambana kuhakikisha unakuwa bora lakini kwa sasa ndiyo unatambulika baada ya kufanya jitihada za kila aina kuufanya uwe ulivyo.”
“Sidhani kama atanitoka kichwani kwangu, naona kama ametutoroka kwa kuwa hatuhitaji aondoke muda huu lakini hakuna jinsi tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” anasema.
Snura Mushi ‘Snura’
Anasema anasikitika sana hasa kwa wao ambao ndiyo kwanza wameingia kwenye muziki na walitaka kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri kama Mangwea, lakini kwa bahati mbaya au nzuri Mungu amechukua kiumbe chake hakuna cha kufanya kupinga hilo kwani haliwezekani.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 2, 2013

4 aaa9f
1 802eb
2 2b5a3

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...