Sunday, June 02, 2013

Wasemavyo wasanii kuhusiana na kifo cha Ngwea

Kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea ambaye amefariki nchini Afrika ya Kusini ambako alikwenda kufanya maonyesho, wasanii mbalimbali  wamezungumzia kifo chake.
Ni dhahiri, Albert Mangwea alikuwa katika kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi na ndiyo uhai wake ulikopotea, Mwandishi wetu Kalunde Jamal aliongea na baadhi ya wasanii wenzake na maongezi yakawa kama ifuatavyo:
Joseph Haule a.k.a Profesa Jay
Anasema katika hili hakuna jinsi kwa kuwa kila binadamu atayaonja mauti.
“Inaniuma sana lakini sina cha kufanya kwa kuwa ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa, kinachotakiwa ni kumuombea apumzike kwa amani  huko aendako.         
Selamani Msindi ‘Afande Sele’
Anasema anamtambua Ngwea siyo kama msanii bali ni mdogo wake wa karibu na ameshindwa kujizuia kutoa machozi kuhusiana na kifo hicho.
Anaongeza kuwa katika kuonyesha ni kwa jinsi gani kijana huyo alikuwa na mapenzi na watu kwani kwao ni Morogoro lakini alijulikana ni kijana wa Dodoma almaarufu East Zoo.
Ngwea kapambana na muziki ukiwa hauna mbele wala nyuma kapambana kuhakikisha unakuwa bora lakini kwa sasa ndiyo unatambulika baada ya kufanya jitihada za kila aina kuufanya uwe ulivyo.”
“Sidhani kama atanitoka kichwani kwangu, naona kama ametutoroka kwa kuwa hatuhitaji aondoke muda huu lakini hakuna jinsi tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” anasema.
Snura Mushi ‘Snura’
Anasema anasikitika sana hasa kwa wao ambao ndiyo kwanza wameingia kwenye muziki na walitaka kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri kama Mangwea, lakini kwa bahati mbaya au nzuri Mungu amechukua kiumbe chake hakuna cha kufanya kupinga hilo kwani haliwezekani.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...