Monday, February 17, 2014

MAMBO MATANO (5) YANAYODIDIMIZA MAHUSIANO NA NDOA...!!!

Makala hii ni tafakari huru kuhusu mambo ya msingi katika mahusiano.  Hapa utapata tafakari ya maana ya maneno na imani ambazo zinatutatiza wengi wetu.

Labda kipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepo mahusiano wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndio ukweli wenyewe.  Ndoa ni namna tuu ambayo wawili walio kwenye mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa wao wapo rasmi katika mahusiano. 
Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namna ya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokea kuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo za ndoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawana mali, n.k. 
Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwa Mungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua.
 Hivyo basi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi. Kiuhalisi inabidi kwanza yawepo mahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume cha hivyo ni kuwa unakula kiapo ‘feki’.
Ndio maana basi, ni muhimu kwa wapenzi kutambua kweli kama wanahitajiana, kuwa kwenye mahusiano na kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka kuweka kiapo rasmi cha kuwa pamoja.
Kutumia ndoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayo pengine yanaweza yasilete faida hapo baadae. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...