Tuesday, March 05, 2013

NICKI MINAJ AWATIMUA WAFANYAKAZI WAKE

Kutokana na kuwepo kwa uvumi wa kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha sura yake Nicki Minaj awatimuwa kazi watengeneza nywele pamoja na wapambaji wake muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani

Nicki amewatimuwa wafanyakazi wake hao siku moja baada ya rapa huyo kusema kwamba hajafanyiwa upasuaji wowote wa kurekebisha sura yake

Chanzo cha habari kinasema kuwa "Nicki anajaribu kutengeneza hali ambayo watu wanamuheshimu kama msanii amemfukuza kazi mtengeneza nywele wake wa muda mrefu"

"Nicki anaamini kwamba sasa amemalizana na masuala ya American Idol hivyo watu wataanz kumuangalia kwa jicho la tatu kipindi hiki ambacho anapanga kutoa albamu yake mpya ya Hip Hop

Uchaguzi wa rais nchini Kenya Uhuru Kenyatta aendelea kuongoza huku bado kura zikiwa bado zinaendelea kuhesabiwa.


Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya  Jumatatu.
Maafisa wa uchaguzi wamesema zaidi ya asilimia 70 ya watu milioni 14.3 waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza katika uchaguzi huo.
Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa kisiasa wa Jubilee Bw.  Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia 55 dhidi ya mpinzani wake Waziri Mkuu Raila Odinga wa muungano wa kisiasa wa CORD akiwa na asilimia 40.
Hata hivyo, muungano wa CORD tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu matokeo hayo na kutilia shaka mfumo mzima wa utoaji wa matokeo hayo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya-IEBC Isaack Hassan amesisitiza kuwa matokeo hayo ni ya awali tu.
 Mshindi katika uchaguzi huo, anatakiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura la sivyo wagombea wawili wa juu watalazimika kuingia katika awamu pili ya uchaguzi mwezi Aprili mwaka huu.

SAKATA LA DIAMOND PLATNUM KUMDHURUMU MENEJA WAKE

                                  Raque akiwa na Diamond kwenye interview
Meneja wa Diamond Platnumz, Raqey Mohamed amelazimika kutumia mtandao wa Facebook kukanusha habari iliyoandikwa na gazeti la udaku la ‘Jumatatu’ kuwa ametapeliwa na Diamond. Amesema Diamond ni mchapakazi na mwaminifu na mkataba wao hauhusiani na mtu yeyote.

Raqey ameandika, “this is coming from me Raqey known as Diamond Platnumz Manager, hakuna ukweli wowote juu ya habari hii, Diamond is a hard working kind and loyal. Our contract has nothing to do with anybody. If you want to write a story at least pay a visit to my studio or call me before you write a story.”

Bongo imempigia simu Raqey ambaye ameendelea kusisitiza kuwa habari hiyo ni ya uzushi na ya upuuzi mtupu.

JOHN MNYIKA APANGA KUITISHA MAANDAMANO MAKUBWA MACHI 26


Mbunge wa Jimbo la Ubungo JOHN MNYIKA amesema Ofisi yake imepanga kuitisha Maandamano makubwa Machi 16 Mwaka huu kuelekea Ofisi za Wizara ya Maji, kutokana na Wizara hiyo kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la upatikanaji wa Majisafi pamoja na uondoaji wa Majitaka katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo.
 
Akizungumza na CLOUDS FM, MNYIKA amesema kuwa tayari Ofisi yake imekamilisha hatua za msingi za uratibu wa maandano hayo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Jeshi la Polisi pamoja na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.Endelea kupiti audifacejackson blog ..Amebainisha kuwa licha ya ofisi yake kulifikisha suala la tatizo la Maji katika baadhi ya maeneo ya Jimbo hilo Wizarani sambamba na kuwasilisha hoja Binafsi bungeni, hakuna hatua zozote za awali zilizochukuliwa huku Wakazi wa maeneo hayo wakitaabika kwa kukosa maji.

SHULE INA WALIMU 8 WA KIKE,6 KATI YAO NI WAJAWAZITO WAOMBA MSAADA

SERIKALI imeombwa iwapatie walimu wa kiume Shule ya Msingi Orbili, kutokana na walimu wote wanawake wa shule hiyo kupata ujauzito na hawafundishi hivi sasa.

Ombi hilo limetolewa na wakazi wa Kijiji cha Orbili Kata ya 
Shambarai wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao wakati wakiongea na waandishi wa habari, walisema kuwa shule hiyo ina walimu nane, ambapo wanaume ni wawili na wanawake ni sita, akiwemo Mwalimu Mkuu, wote wana ujauzito.
Walisema walimu wawili wanaume, hawawezi kuwafundisha wanafunzi wote wa shule hiyo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, hasa ukizingatia kuwa darasa la nne na la saba, watafanya mtihani wa Taifa mwaka huu.

Walisema kuwa hivi karibuni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, alijifungua mtoto na walimu wengine watano waliobaki, wanatarajiwa kujifungua wakati wowote.Endelea kupiti audifacejackson blog

Nadhani shule hii ifungwe ili Serikali ilete walimu wengine kwani hawa walimu wenye mimba hawafundishi wanafunzi wetu, wenyewe wamebaki kula udongo na malimao,” alisisitiza mkazi mmoja.

SOURCE::HABARI LEO:

President Kikwete Meets With MCC Officials In Dar Es Salaam.

President Jakaya Mrisho Kikwete greets Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation’s Chief of Staff, who paid him a visit at the State House in Dar es salaam March 4, 2013. Centre is the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.
President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with (from left)  Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation’s Chief of Staff, MCC’s Vice President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock,the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt. and Mr Matt KAvanagh, MCC Resident Country Director ,  who paid him a visit at the State House in Dar es salaam March 4, 2013. Centre is the US Chief of Staff, Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.
President Jakaya Mrisho Kikwete in a group photos with (from left)  Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge Corporation’s Chief of Staff (right) MCC’s Vice President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock (second row right),the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt (front row left) Mr Matt KAvanagh, MCC Resident Country Director (second row left) and the Minister for Finance Dr Willim Mgimwa and Mr Bernard Mchomvu, the CEO of the Millenium Challenge Account (MCA) -Tanzania,  at the State House in Dar es salaam  March 4, 2013. Centre is the US Chief of Staff, Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.(STATE HOUSE PHOTO)

BIFU LA WEMA SEPETU NA AUNTY EZEKIEL!! BIFU: AUNT EZEKIEL NA WEMA SASA..

Wacheza filamu wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wadaiwa kuwa na bifu kubwa kwa sasa. inasemekana bifu hilo lilianza kwenye mkesha wa mwaka mpya baada ya aunt kutofika kwenye sherehe ya kukaribisha mwaka mpya iliyoandaliwa nyumbani kwa Wema licha ya kukubali mwaliko. 


Ilipotimu saa 6:01 usiku bila ya Aunt kuonekana, Wema alimtumia ujumbe mzito kupitia BBM na Aunt akaanza kuomba radhi na ujumbe wa Wema ulisomeka hivi: “Hata sina hamu na wewe ila Happy New Year, sihitaji samahani yako sijui niku-delete?”akimaanisha amfute BBM.


Inasemekana Wema alikasirika na kuhisi kwamba Aunt aliungana na baadhi ya wasanii wengine wa Bongo Movie ambao hakuwaalika kwenye shughuli yake kutokana na kupishana nao 
Kiswahili siku za nyuma.


Asubuhi ya mwaka mpya, Aunt aliandika kwenye mtandao wa BBM maneno ya kuomba radhi kwa wema; “ Chondechonde my luv, nimekosea mamy naomba unisamehe, naomba msamaha mbele ya hadhara.”. juhudi za kuomba radhi azikuzaa matunda kwan Wema hakujibu kitu zaidi ya kumpotezea rafiki yake huyo

MSANII MWINGINE BONGO MOVIE MBURULAS. VIDEO INAYOMUONESHA MSANII WA FILAMU BONGO ( SHAMSA FORD) AKIJIFUNGUA YAVUJA NA KUSAMBAA...



VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali. 
 
Akizungumzia  suala hilo  hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo msanii huyo alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo. 
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” kilisema chanzo hicho 
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Shamsa ambaye alisema:“Kiukweli nimeumia sana, hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”
Source-mpekuzi

UCHAGUZI WA KENYA MATOKEO YA AWALI


Kenya Elections 2013 Presidential provisional results


Uhuru Kenyatta (TNA) 663,855 (55.95%)


Raila Odinga (ODM) 473,598 (39.91%)

Mudavadi (UDF) 30,148 (2.54%)
Kiyiapi (RBK) 4,553
Kenneth (Eagle) 6,177
Karua (Narc Kenya) 4,333
Dida (ARC) 2,619

Muite (Safina) 1,316

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...