SERIKALI
imeombwa iwapatie walimu wa kiume Shule ya Msingi Orbili, kutokana na
walimu wote wanawake wa shule hiyo kupata ujauzito na hawafundishi hivi
sasa.
Ombi hilo limetolewa na wakazi wa Kijiji cha Orbili Kata ya
Shambarai wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Wakazi
hao ambao hawakutaka kutaja majina yao wakati wakiongea na waandishi wa
habari, walisema kuwa shule hiyo ina walimu nane, ambapo wanaume ni
wawili na wanawake ni sita, akiwemo Mwalimu Mkuu, wote wana ujauzito.
Walisema
walimu wawili wanaume, hawawezi kuwafundisha wanafunzi wote
wa shule hiyo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, hasa ukizingatia
kuwa darasa la nne na la saba, watafanya mtihani wa Taifa mwaka huu.
Walisema
kuwa hivi karibuni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, alijifungua mtoto na
walimu wengine watano waliobaki, wanatarajiwa kujifungua wakati wowote.Endelea kupiti audifacejackson blog
“Nadhani shule hii
ifungwe ili Serikali ilete walimu wengine kwani hawa walimu wenye mimba
hawafundishi wanafunzi wetu, wenyewe wamebaki kula udongo na malimao,” alisisitiza mkazi mmoja.
SOURCE::HABARI LEO:
No comments:
Post a Comment