Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu.
Maafisa
wa uchaguzi wamesema zaidi ya asilimia 70 ya watu milioni 14.3
waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza katika uchaguzi huo.
Matokeo
ya awali yanaonyesha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa kisiasa wa
Jubilee Bw. Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia 55 dhidi ya mpinzani
wake Waziri Mkuu Raila Odinga wa muungano wa kisiasa wa CORD akiwa na
asilimia 40.
Hata
hivyo, muungano wa CORD tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu matokeo
hayo na kutilia shaka mfumo mzima wa utoaji wa matokeo hayo.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya-IEBC
Isaack Hassan amesisitiza kuwa matokeo hayo ni ya awali tu.
Mshindi
katika uchaguzi huo, anatakiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura la
sivyo wagombea wawili wa juu watalazimika kuingia katika awamu pili ya
uchaguzi mwezi Aprili mwaka huu.
No comments:
Post a Comment