Thursday, January 09, 2014

SAMAKI MKUBWA AINGIA SEHEMU ZA SIRI ZA BINTI HUKO BUNDA ...!!!

MAISHA ya mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 12, (jina tunalihifadhi), anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Bwanza, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, yako hatarini baada ya kurukiwa na samaki aina ya sato, kuingia sehemu ya siri na kukimbilia tumbani.

Tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu, saa 11 alfajiri,wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani ya nyanya, vitunguu iliyopo kandokando ya ziwa hilo.

Akizungumza na Majira, kaka wa mtoto huyo (jina tunalihifadi), mwenye miaka 31, alisema tukio hilo limewashangaza wakazi wa Kijiji cha Bwanza na vitongoji vyake.

Alisema mdogo wake alikuwa akichota maji katika ziwa hilo akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini, kuingia sehemu yake ya siri na kukimbilia tumboni.

"Mdogo wangu alifanya jitihada za kumvuta ili aweze kumtoa lakini alikimbilia tumboni na kuanza kupata maumivu makali, kutokwa na damu nyingi baada ya kuparazwa na miba ya
mgongo wa samaki huyo.
 

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

GOOGLE YATAJA WATU MAARUFU WA TANZANIA AMBAO PICHA ZA ZILITAFUTWA SANA KWENYE MTANDAO MWAKA 2013

trends
Google trends imetoa list ya majina/maneno ambayo yametafutwa sana kwenye mtandao wa google search kwa mwaka 2013.
Dunia nzima ime-search sana jina la Nelson Mandela likifuatiwa na Paul Walker.
Upande wa Tanzania majina ya watu maarufu yaliyotafutwa sana kwa upande wa picha(image search) ni
Wema,Diamond na Wema Sepetu.
Kwa ujumla unaweza kusema jina lililotafutwa sana kwa upande wa image search kwenye google kwa mwaka 2013 ni Wema Sepetu
google

 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

BASI LA MTEI LACHOMWA MOTO NA WANANCHI LIKIWA SAFARINI

Screen Shot 2014-01-09 at 9.07.49 PM
Hii ni ajali ambayo imetokea njia Panda ya kwenda Arusha kama unatokea Singida, wakazi wa eneo hilo wamechoma moto basi la Mtei ambapo waandishi wameongea na miongoni mwa mashuhuda na abiria wa ajali hiyo na wametoa haya maelezo hapa chini.
mamtei
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 08, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAJINA ZAIDI 5,400 YAWANIA UJUMBE WA BUNGE LA KATIBA



Balozi Ombeni Sefue
********
Serikali imeanza mchakato wa kuchambua asasi na majina ambayo atakabidhiwa Rais, kuwa miongoni mwa wajumbe watakaounda Bunge maalumu la Katiba.

Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema, jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshawasilisha mapendekezo yao ya majina takribani 5, 400, Ikulu.

Kuhusu kutaja baadhi ya majina ambayo asasi hizo zimeyependekeza kwenda Ikulu, Balozi Sefue, alisema ofisi hiyo haina ruhusa ya kufanya hivyo labda asasi zenyewe ziamue kufanya hivyo kupitia vyombo vya habari.

“Jumla ya asasi 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, zimeshaleta majina ya watu 5, 400 zilizoyapendekeza. Mapendekezo yaliyoletwa ni mengi, kwani katika idadi hii, wanaotakiwa ni 2001, hivyo kazi ipo,” alisema na kuongeza:

“Kuhusu majina yaliyopendekezwa, hatuna ruhusa ya kufanya hivyo, labda kwa ridhaa yao wenyewe wanaweza kutangaza kwenye vyombo vya habari. Na sasa kazi tunayoendelea nayo ni uchambuzi wa majina hayo ili tumpelekee Rais, ambaye ndiye atakayejua watakaopaswa kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge la Katiba.” 
CHANZO: NIPASHE 

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...