Tuesday, September 02, 2014

SASA UKICHUKUA FEDHA BENKI ROHO MKONONI


Katuni inayoonyesha ujambazi wa kutumia pikipiki na bastola unavyoshika kasi jijini Dar es Salaam. 

Ni roho mkononi. Hayo ndiyo maneno matatu yanayofaa kuelezea hali ilivyo jijini Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa pale mtu anapobeba fedha nyingi.
Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa, kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.
Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupata taarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.
Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum Mashati alisema: “Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka benki. Eti majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa una kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”
Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo Mlimani City, ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai hayo... “Si kweli kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya uhalifu huu. Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu wanapohudumia wateja.
“Hata mteja anapoingia benki hukatazwa kuongea na simu au kuandika ujumbe. Mazingira tuliyojiwekea hayaruhusu kabisa mawasiliano kati ya benki yetu na watu wa nje wakati wa kazi. Nadhani vitendo hivi vya ujambazi vinaanzia kwa wateja wenyewe kutoa taarifa juu ya mipango yao kwa watu ambao si waaminifu,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAY DEE "MAADUI ZANGU WAMEBADILISHA WIMBO"


Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee  

 Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.
Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.
Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.
Habari hiyo inahusishwa na kile kilichodaiwa kuwa mwanamuziki huyo ameachana na mume wake, Gadner G Habash, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio Times FM. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NDEGE YA KENYA YAANGUKA TANZANIA


Masalia ya ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited iliyoanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuua watu watatu jana.
Ndege ya Kampuni ya Safari Express Limited imeanguka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwateketeza watu watatu waliokuwamo ndani.
Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia.
Meneja wa Udhibiti wa JKIA, Clever Davor aliliambia gazeti la Daily Nation la Kenya kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada ya uwanja huo ikiwa imeruka angani urefu wa futi 14,000. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM WAUTEKA MJI MUHIMU NIGERIA

Wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
Kundi la Boko haram limefanya mashambulizi katika mji wa Bama na kusababisha mauaji ya watu wengi huku wengine wakitoroka.
Wanamgambo hao waliuteka mji wa Bama ,ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno siku ya Jumatatu baada ya jaribio la awali la kutaka kuuteka mji huo kuzimwa na vikosi vya serikali.
Akizungumza na BBC ,wakaazi wamethibitisha kuwa mji huo umetekwa na kundi hilo na kwamba maelfu ya watu sasa wameachwa bila makao.
Mamlaka ya Nigeria bado haijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Taarifa zinasema kuwa watu wengi wametoroka wakiwemo wanajeshi.
Zana za kivita zinazotumiwa na wapiganaji wa Boko Haram
Hapo awali jeshi la Nigeria lilitoa ripoti kuonyesha kuwa mpaka sasa limewaua wapiganaji 70 wa Boko Haram ,kutokana na mapigano kati ya kikundi hicho na wanajeshi Kaskazini -Mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo kwa magari ya kivita.Taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kuwa wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnesty International limetoa takwimu kuwa raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.

KIONGOZI WA AL-SHABAB ASHAMBULIWA

Haijulikani ikiwa Ahmed Abdi Godane aliuawa kwenye shambulizi hilo
Wanajeshi wa Mreakani wamefanya mashambulizi ya angani dhidi ya msafara wa magari ya mmoja wa viongozi wa kundi la Al Shabaab nchini Somalia.
Haijulikani ikiwa kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Abdi Godane aliuawa kwenye shambulizi hilo lililofanyika umbali wa kilomita 240 kusini ya mjini mkuu Mogadishu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wanajeshi wa Marekani walionekana wakishuka katika eneo hilo kwa helikopta na kuchukua miili ya wapiganaji waliouawa.
Msemaji wa idara ya ulinzi ya Marekani, (Rear Admiral John Kirby) alisema bado inadurusu matokeo ya shambulizi hilo.
Baadhi ya taarifa zinasema kuwa wapiganaji waliwakamata wakazi walioshukiwa kutoa taarifa kwa Marekani.

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...