Tuesday, September 02, 2014

JAY DEE "MAADUI ZANGU WAMEBADILISHA WIMBO"


Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee  

 Malkia wa muziki wa R&B, Lady Jay Dee amedai kuwa maadui zake wamebuni njia mpya ya kumwangusha, baada ya zile za awali kutofanikiwa.
Katika waraka mrefu aliouandika katika mtandao wa facebook, Lady Jay Dee alisema watu wasiopenda mafanikio yake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kumwangusha, lakini hata hivyo wameshindwa.
Jay Dee analalamikia habari iliyoandikwa juu yake kuwa amekuwa katika uhusiano mpya na kijana aliyemzidi umri, jambo analosema halina ukweli.
Habari hiyo inahusishwa na kile kilichodaiwa kuwa mwanamuziki huyo ameachana na mume wake, Gadner G Habash, ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio Times FM. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Jide ameandika: “Hata kama nimeachana na mume wangu, siyo sababu ya kunihusisha katika uhusiano na mwanamume mwingine yeyote. Habari hii imenivunjia heshima. Nafikiri lengo la uzushi huu ni kumfanya Lady Jaydee aonekane mtu asiyefaa.”
Habari hiyo ilipambwa na picha ambazo alizipiga mwenyewe kwa kutumia simu ya mume wake.
Aliongeza: “Ni vizuri kuzusha vitu ambavyo angalau unavijua, hizi picha zilipigwa kwa simu ya Gadner ambaye mnasema nimeachana naye, hamuoni kama mnawadanganya watu?”
Aliongeza kuwa huenda aliyeanzisha habari hizo ameona zile ambazo zilikuwa zikivuma wakati fulani, zimeshuka chati.
Alihoji: “Je, wimbo Jay Dee mgumba, Jay Dee tasa umeshuka chati ndiyo maana mmeamua kuleta mwingine?”
Hata hivyo, alisema lengo la wanaoanzisha uzushi juu yake ni kumdhoofisha lakini anaamini jinsi alivyoshinda vita ya kwanza, atashinda tena vita ya pili. “Hata kama ndoa yangu haiko sawa, niacheni.
Lakini isiwe sababu ya kuendelea kunichafua kwa maneno ya kizushi. Siyo lazima niandikwe, kwa sababu nilikuwapo kabla ya kuandikwa sana... nitaendelea kuwapo bila kuandikwa.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...