Thursday, November 07, 2013

POLISI WAFANYA JARIBIO KATIKA HOTELI YA GOLD CREST MWANZA KUONA JINSI WANANCHI WANAVYOWEZA KUJIAMI NA MATUKIO YA UVAMIZI

WAPINGA MAREKEBISHO SHERIA YA MAGAZETI


lissu_5a412.jpg
Wakati Serikali imewasilisha muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Magazeti, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imepinga marekebisho ya sheria hiyo kwa madai kuwa hayakufanyiwa tafakuri na utafiti.
Akiwasilisha maoni hayo bungeni jana, Msemaji wa Kambi hiyo kuhusu Sheria, Tundu Lissu, alisema mapendekezo hayo yamefikishwa bungeni bila kufanyia tafakuri au utafiti wowote.
"Mwanasheria Mkuu wa Serikali angefanya utafiti kidogo tu angegundua kwamba kifungu cha 55 hakina na hakijawahi kuwa na, sababu yoyote ya kuendelea kuwepo katika kanuni ya adhabu,"alisema .
Alisema hiyo inatokana na kifungu hicho hicho kutungwa upya, kwa maneno yale yale, kama kifungu cha 31 cha Sheria ya Magazeti kwamba kifungu hicho hakikupaswa kuwepo kwa sababu, makosa ambayo kifungu hicho kinafafanua hayako tena kwenye kanuni ya adhabu na badala yake, yako katika Sheria ya Magazeti.
"Inaelekea katika fasta fasta ya kupitisha muswada wa Sheria ya Magazeti, kifungu cha 55 kilisahauliwa katika kanuni ya adhabu wakati vifungu vyote vinavyohusu makosa ya uchochezi na kashfa ya kijinai vilipohamishiwa katika Sheria ya Magazeti,"alisema Lissu.

MBUNGE WA UKEREWE AFUTIWA DHAMANA NA KUAMRIWA AENDE SELO SIKU 14

560843761_fd884.jpg
Na mwanahabari Bundala William
DHAMANA ya mbunge wa jimbo la Ukerewe, Salvatory Machemli (CHADEMA) imefutwa na ameamuriwa na mahakama kwenda rumande siku 14 kwa kuwa wadhamini wake wamekosa sifa baada ya mshitakiwa na wadhamini wake watatu kushindwa kufika mahakamani ili kuwezesha kesi inayomkabili kusikilizwa kama ilivyopangwa.
Pia, Mbunge huyo ametakiwa kuwasilisha vitambulisho vyake katika kituo cha polisi na amezuiliwa kutoka nje ya wilaya bila kibali cha mahakama.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo Faustine Kishenyi ametoa uamuzi huo leo baada ya upande wa mashitaka kuomba mshitakiwa afutiwe dhamana.


Wadhamini ambao ni Shellifu Ngelezya, Max Mhogo na Konsolata Machemli wamepoteza sifa hivyo udhamini wao umefutwa.
Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, Inspekta Samweli Onyango amesema mshitakiwa kwa makusudi ameshindwa kufika mahakani zaidi ya mara tano bila kutoa taarifa wakati kesi yake ikitajwa.

MATOKEO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

ARSENAL YAIKALISHA BORUSSIA DORTMUND, ETO'O APIGA MBILI CHELSEA IKIUA WAJERUMANI...MESSI KAMA KAWA, AIPIGIA MBILI BARCA IKIINYANYASA AC MILAN ULAYA
article-2488571-193C99A200000578-202_634x431_c6de5.jpg
Zama za ushindi: Aaron Ramsey (kulia) na Mesut Ozil wakishangilia bao pekee la ushindi la Arsnal
BAO pekee la Aaron Ramsey dakika ya 62, limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Borussia Dortmund nchini Ujerumani.
Hilo linakuwa bao la 13 kwa mchezaji huyo msimu huu na bao la tano katika michuano ya Ulaya msimu huu. Pamoja na kufungwa, wenyeji ndio waliocheza vyema usiku huu na kabla ya Arsenal kupata bao lake, hawakuweza kutengeneza nafasi hata moja ya kufunga.
Borussia ambayo inapewa sifa ya moja ya timu bora kabisa Ulaya kwa sasa, iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Stuttgart katika ligi ya kwao, Bundesliga, lakini ilikalishwa na mtutu mmoja wa bunduki.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...