Tuesday, April 19, 2016

MAGUFULI ATINGA CRDB KAMA RAIA WA KAWAIDA...!!!

Rais John Pombe Magufuli akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland baada ya kumaliza shughuli iliyompeleka.

Rais John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mkono wakati akiondoka katika benki ya CRDB, Tawi la Holland. 

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

ANGALIA PICHA ZA MUONEKANO WA DARAJA LA JIPYA LA KIGAMBONI


Hatimaye ile ndoto ya muda mrefu ya Watanzania kuona daraja la Kigamboni likikamilika imewadia baada ya ujenzi ulioanza mwaka 2012 kukamilika na kesho Aprili, 19 linataraji kuzinduliwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.


Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 19, 2016

20160419_042717 20160419_042731 20160419_042751
Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

WANAFUNZI WATATU WA KIDATO CHA SITA WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUIBA SHULENI



Jeshi la Polisi mkoani Singida linawashikilia wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari Mwenge mjini hapa kwa tuhuma za kuvunja na kuiba vitu mbalimbali kwenye ofisi ya usajili wa wanafunzi katika shule hiyo vinavyokadiliwa kuwa na thamani ya Milioni 1.5.
Kamanda wa Polisi wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja wanafunzi hao ambao wote ni wa kidato chasSita kuwa ni Emmanuel Mwita (19), Erick Dotto (21) na Pasua Lawrence (20).

Kwa mujibu wa Kamanda Sedoyeka, tukio hilo lilitokea Aprili, 16 mwaka huu majira ya saa 3.30 usiku ambapo inadaiwa wanafunzi hao baada ya kuvunja ofisi hiyo waliiba seti moja ya Kompyuta, “flash disk” yenye ukubwa wa GB 8, “Extension Cable” na rimu 51 za karatasi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

KANE HAKAMATIKI KWA KUTUPIA NYAVUNI EPL

Harry Kane 4
Harry Kane alikuwa miongoni mwa nyota wakati Spurs ikipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke jana usiku kwenye dimba la Britania baada ya kuifungia timu yake magoli mawili na kuendeleza ubora wake kwenye ligi msimu huu.

Inafurahisha kuona jamaa alianza ligi kwa ukame wa magoli katika mechi kadhaa na baadhi ya watu kuanza kumsema yeye ni mchezaji wa ku-shine kwa msimu mmoja. Mshambulizi huyo wa England ameendelea kujitengenezea soko na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakao gombewa kwa mkwanja mrefu wakati wa usajili wa dirisha la majira ya joto.
Bayern Munich na Real Madrid inasemekana kuwa ni klabu mbili kubwa zinazofukuzana kumsaini lakini pia inasemekana Aston Villa wanataka kuuza washambuliaji wao wote na kuvunja benki kwa ajili ya kuinasa saini ya mpachika mabao huyo.

Magoli yake mawili ya jana dhidi ya Stoke yamemfanya afikishe jumla ya mabao 24 na kuongoza orodha ya wapachika mabao akifatimwa na Jamie Vardy wa Leicester mwenye magoli 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

TOTTENHAM YAISOGELEA LEICESTER CITY, YAIPIGA STOKE CITY 4-0

Mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza umeendelea usiku wa Jumatatu ambapo Stoke City ilikuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika uwanja wake wa nyumbani wa Britannia.

Mchezo huo umemalizika kwa wenyeji Stoke City kumaliza mchezo huo kwa kupokea kipigo kutoka kwa Totenham Hotspur cha goli 4-0, magoli ya Tottenham yakifungwa na Harry Kane aliyefunga magoli mawili dk. 9 na 71 na mengine mawili yakifungwa na Dele Alli dk. 67 na 82.

Baada ya matokeo hayo, Tottenham imefikisha alama 68 ikiwa nyuma kwa alama tano na viongozi wa ligi, Leicester City ambao wana alama 63, kwa upande wa Stoke City wao wamemesalia katika nafasi ya tisa ya msimamo wakiwa na alama 47. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...