Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Ikulu
ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa
televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi
kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.
Inatarajiwa
kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba
kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake
wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo. Rais Obama amesema
hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba
yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya
mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima
ya afya. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Raia wengi kutoka Ulaya wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria
Mwanamke
mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari
iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua
mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.
Monique
alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha
kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye
asili ya Uholanzi na Uturuki. Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS. Aicha
,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia
wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi
Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Jules Bianchi dereva wa F1 wa timu ya Marussia
aliyepata ajali katika mashindano ya Japanese Grand Prix Oktoba,5, 2014
Dereva
wa magari ya langa langa ya Formula 1 Jules Bianchi ametoka katika hali
ya kuwa mgonjwa mahututi na sasa anapua bila msaada wa mashine,
wamesema wazazi wake katika taarifa yao.
Dereva huyo wa timu ya
Marussia mwenye umri wa miaka 25, alijeruhiwa kichwani alipoligonga gari
la kuvuta magari katika michuano ya Japanese Grand Prix Oktoba 5,2014. Dereva
huyo raia wa Ufaransa amehamishwa kutoka hospitali ya mjini Yokkaichi
nchini Japan na kupelekwa katika hospitali ya Nice nchini Ufaransa kwa
uchunguzi zaidi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Timu ya Algeria wakishangilia ushindi wa timu
yao kufuzu kucheza fainali za Caf 2015 nchini Equatorial Guinea
Matumaini
ya eneo la Afrika Mashariki kuwa na timu angalau moja katika fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea
mwaka 2015, yameyeyuka baada ya mwakilishi pekee wa eneo hilo timu ya
Uganda kucharazwa na Guinea
mabao 2-0 katika mchezo wa kundi E uliofanyika mjini Casablanca, Morocco, Jumatano.
Timu ya Nigeria mabingwa watetezi hawatashiriki fainali za Caf 2015 baada ya kutolewa katika makundi
Uganda iliyokuwa na pointi 7 kama Guinea ilitakiwa kushinda mchezo huo. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 11. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Sepp Blatter, rais wa FIFA akiitangaza Qatar kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022
Mfichua
siri kuhusu tuhuma za rushwa kutolewa na Qatar ili kuiwezesha nchi hiyo
kushinda nafasi ya kuandaa Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022
ameiambia BBC kuwa anaishi kwa hofu kutokana na hatua yake hiyo.
Mwaka
2011, Phaedra al-Majid alidai kuwa maafisa wa Qatar walijitolea
kuwalipa maafisa watatu wa vyama vya soka barani Afrika kiasi cha dola
milioni moja na nusu ili kuiunga mkono Qatar kuwa mwenyeji wa michuano
hiyo mikubwa duniani.
Baadaye Bi Phaedra al-Majid aliondoa tuhuma
hizo, lakini sasa anasema alilazimishwa kubadili kauli yake. Anasema
ameingia katika hali ya uendawazimu ya "kujiona anaonewa kila wakati,
hofu na vitisho" (na kwamba atajiona mkosaji maisha yake yote.)
Kamati
ya Qatar ya uandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia imesema ushahidi wa
Phaedra al-Majid ulitiliwa mashaka na timu ya uchunguzi ya FIFA, na
kwamba tuhuma zote zilichunguzwa na kutupiliwa mbali. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz