Habari kutoka kwa chanzo cha uhakika zinadai kuwa msanii wa zamani wa
kundi Daz Nundaz na hitmaker wa ‘Figure Namba 8′ Daz Baba
amechanganyikiwa kutokana na hivi karibuni kuonekana akifanya vitendo
ambavyo havilingani na mtu mwenye akili timamu.
Chanzo hicho kimesema Daz alionekana maeneo ya Morogoro akiwa katika
hali iliyowatia mashaka ndugu, mashabiki wa muziki pamoja na wasanii
wenzake.
Rafiki wa karibu na Daz Baba amemwambia mwandishi wetu jana akiwa mkoani
Morogoro kuwa hali ya msanii huyo ni mbaya na ana dalili zote za mtu
ambaye ni Kichaa na amekuwa mtu wakuzunguka barabarani huku akifanya
matukio ya ajabu.
Msikiti
mkubwa wa barabara ya saba mjini Dodoma umewaka moto mchana huu
ikiwa ni muda mfupi baada ya swala ya mchana kumalizika....
Akiongea
kwa njia ya simu na Mwandishi wetu, mmoja wa mashuhuda
walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni
moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la
msikiti huo...
Kwa
mujibu wa shuhuda huyo, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na
jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha
kutokana na
moto huo.
 |
| Picha ya maktaba: |