Tuesday, June 04, 2013

Jokate aongea baada ya Diamond kukiri kuwa anajuta kumkosea na kuuvunja moyo wake

Hivi karibuni Diamond aliamua kuweka ‘ego’ pembeni na kukiri kuwa Jokate Mwegelo ndiye msichana katika maisha yake aliyemkosea sana na anajuta kumuumiza
Diamond alifunguka hayo kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, kilichorushwa wiki iliyopita.

Akiongelea jinsi alivyomuumiza Jokate, Diamond alisema, “Kwasababu alikuwa too innocent halafu hakuwahi kunikosea kitu chochote Jokate kabisa, halafu nikamwingiza kwenye matatizo, watu wakamchukulia tofauti kwamba ‘Jokate kamchukulia Wema boyfriend wake’ wakati nilimfuata mimi kama mimi, nilimtafuta mwenyewe halafu then nikawa niko naye halafu ghafla nikarudisha mahusiano kwa Wema. Sikujiskia vizuri halafu still haikuwa vizuri so sometimes nikikaaga hivi nasema nilimkosea.”

Akijibu swali la kwanini alimuacha Jokate, Diamond aliongeza, “Sijui nilirogwa hata sijui, I don’t know, sijui hata kwanini, hakuwahi kunikosea chochote sio, sababu nilikuwa nikikaa naye alikuwa akinishauri vitu vingi vya maendeleo, sijui ulikuwa ni utoto sielewi yaani, sijui ni kitu gani, nilijikisa vibaya sana, halafu mtoto wa watu mstaarabu sana, alijitahidi kujenga career yake sasa hivi imekaa vizuri.”

Bongo5 imewasiliana na Jokate ili kutaka kufahamu upande wake baada ya kusikia kauli ya Diamond aliyesema anafurahi kuona Diamond amefunguka ukweli.

“Watu wengi hawajui the real issue, I’m glad kama ame-acknowledge I was innocent in that whole matter,” amesema Jokate.

MAPOKEZI YA MANGWEA JIJI ZIMA LAZIZIMA

 Gari iliyobeba mwili wa Albert Mangwea ikisukumwa na washabiki,wapenzi ndugu jamaa na marafiki mara baada kuanza kuondoka eneo la Eapoti hivi punde wakielekea Muhimbili kwa taratibu nyingine,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi--Amen

ANGALIA PICHA MWILI WA ALBERT MANGWEA ULIVYOWASILI DAR

Gari maalum la Kubeba Mwili wa Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Marehemu Albert Mangwea likiwa tayari  kwa kubeba mwili.
Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Wadau kibao wapo uwanjani hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.
Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya habari uwanjani hapa.

ANGALIA PICHA ZA MWANAMKE AZAA WATOTO WATANO KWA MPIGO NCHINI CZECH.

Mmoja wa watoto wa watano akiwa amejifungua mbele ya uangalizi wa jopo la madaktari siku ya jumapili nchini Czech.
Jopo la madaktari wakimchunguza mwanamke Alexandra Kinova miaka 23.
Alexandra Kinova kipindi cha ujauzito.

MAMA NA MPENZI WAKE WAMUUA MTOTO WA MIAKA 4 ILI WAFAIDI PENZI LAO

Wakati mwingine unaweza kudhani binadamu tunageuka kuwa wanyama, lakini huu sio mfano tosha kwani hata wanyama wakali kama simba huwa na huruma na huwalinda watoto wao hadi kufa, baadhi ya binadamu wamekuwa na roho ya ukatili isiyo ya kawaida hata kwa mtoto waliyemzaa wenyewe.
Huko Uingereza mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Magdelena Luczack na mpenzi wake Mariusz Krezolek ambao walihamia uingereza wakitokea Poland, wamefikishwa katika mahakama kuu mjini Birmingham wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji. 
Watu hao wanashtakiwa kwa kushirikiana kumuua kwa kumtesa wka vipigo na  kumyima chakula  kwa makusudi mtoto Daniel aliyekuwa na umri wa miaka minne tu,aliyefariki mwezi march mwaka jana akiwa na jeraha kichwani.
Magdalena ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo anatuhumiwa kushirikiana kwa karibu na baba wa kambo wa mtoto huyo kusababisha kifo chake wakiwa na nia ya kutafuta amani na utulivu katika nyumba yao.

M2 THE P ANA USHAHIDI WOTE KATIKA KIFO CHA ALBERT MANGWAIR.

 
Na Mwandishi Wetu
MBIVU na mbichi sasa zinaweza kujulikana, kinachoombwa ni muda tu, kwani mng’amuzi halisi kuhusu kifo tata cha mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’, yupo kwenye mazingira mazuri kueleza kilichotokea.

KWA NINI ANA USHAHIDI WOTE?
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya mwisho nchini Afrika Kusini.
M2 The P, alipatwa na matatizo sawa na marehemu Ngwea, isipokuwa mwenzake ilifikia hatua mbaya na kupoteza maisha huku yeye akibaki mahututi kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya St. Helen Joseph, jijini Johannesburg nchini humo.
Jambo la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo  alipokwenda kwenye shughuli zake.

JAWABU LA SUMU 
Moja ya mambo yanayozungumzwa pembeni ni kwamba kuna uwezekano mkubwa marehemu Ngwea na M2 The P  waliwekewa sumu kwenye chakula au kupuliziwa ‘laivu’ kisha kutokea yaliyotokea, lengo likiwa kuwadhulumu mzigo wa fedha nyingi waliokuwa nao, hivyo kupona kwa mmoja huyo ni matakwa ya Mungu ili awe shahidi namba moja wa kifo cha Ngwea.

H0TUBA YA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA KATIBA NA YALIYOMO KWENYE RASIMU HIYO NI HAYA HAPA .....



warioba 89a51
1.0. UTANGULIZI
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.
Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.

Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao 1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya wananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano ya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume, Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 04, 2013

1 c2a93
17 cdc7f

VITI MAALUMU VYAFUTWA, UBUNGE KUWA NA UKOMO


Tume ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya Katiba Mpya ukomo wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu bungeni.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph Warioba alisema jana, wanapendekeza kwamba ubunge uwe na ukomo wa vipindi vitatu vya miaka mitano, mitano akimaanisha kwamba kipindi cha mtu kuwa mbunge hakiwezi kuvuka miaka 15.

Rasimu hiyo ya Katiba imependekeza kutokuwapo tena kwa Viti Maalumu na badala yake, imetaka kuwapo kwa nafasi tano za uteuzi zibaki kwa Rais ambazo zitahusisha makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pekee.

Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa
majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...