Tuesday, June 04, 2013

MAMA NA MPENZI WAKE WAMUUA MTOTO WA MIAKA 4 ILI WAFAIDI PENZI LAO

Wakati mwingine unaweza kudhani binadamu tunageuka kuwa wanyama, lakini huu sio mfano tosha kwani hata wanyama wakali kama simba huwa na huruma na huwalinda watoto wao hadi kufa, baadhi ya binadamu wamekuwa na roho ya ukatili isiyo ya kawaida hata kwa mtoto waliyemzaa wenyewe.
Huko Uingereza mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Magdelena Luczack na mpenzi wake Mariusz Krezolek ambao walihamia uingereza wakitokea Poland, wamefikishwa katika mahakama kuu mjini Birmingham wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji. 
Watu hao wanashtakiwa kwa kushirikiana kumuua kwa kumtesa wka vipigo na  kumyima chakula  kwa makusudi mtoto Daniel aliyekuwa na umri wa miaka minne tu,aliyefariki mwezi march mwaka jana akiwa na jeraha kichwani.
Magdalena ambae ni mama mzazi wa mtoto huyo anatuhumiwa kushirikiana kwa karibu na baba wa kambo wa mtoto huyo kusababisha kifo chake wakiwa na nia ya kutafuta amani na utulivu katika nyumba yao.
Mwendesha mashtaka wa serikali Jonas Hankin ameiambia mahakama hiyo kuwa ujumbe wa njia ya simu uliopatikana ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa washtakiwa walikuwa na nia ya kumuua mtoto huyo.
Amesema katika moja ya ujumbe uliutumwa unaonesha kuwa mwezi February mama wa mtoto huyo alimtumia mpenzi wake ujumbe uliosema, “amepoteza fahamu(Mtoto) kwa muda kama vile nimemzamisha kwenye maji. Sasa ninapata muda wa utulivu.”
Mwezi October mwaka juzi kuna ujumbe ambao Krezolek ambae ndie baba wa kambo wa mtoto Daniel, alimtumia ujumbe mama wa mtoto huyo uliosomeka, “Mpeleke (mtoto) kwenye chumba na umfungie huko. Utakuwa na amani na unisubirie mimi.”
Na siku nyingine alimtumia mpenzi wake  ujumbe kuwa, “Tutadili na Daniel akitoka shule, hatapata muda wa kuona wadudu kabisa.”
Mwendesha mashtaka huyo wa serikali ameiambia mahakama kuwa ushahidi mwingine wa wazi ni kwamba inaonekana kuwa March 2 mwaka jana majira ya saa 10:34 jioni wakati mtoto huyo akiwa bado yuko hoi, mama yake alimtumia ujumbe mpenzi wake kwa lugha ya kipolish ukimaanisha, “atapona kufikia kesho, hakuna haja ya kujipa stress na kuita ambulance kwa kuwa hiyo ndiyo italeta tatizo zaidi.”
Washitakiwa hao wamekana mashtaka yote na kurudishwa rumande, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na kumalizika ndani ya wiki nane, hii ikiwa ni wiki ya kwanza.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...