Tuesday, June 04, 2013

M2 THE P ANA USHAHIDI WOTE KATIKA KIFO CHA ALBERT MANGWAIR.

 
Na Mwandishi Wetu
MBIVU na mbichi sasa zinaweza kujulikana, kinachoombwa ni muda tu, kwani mng’amuzi halisi kuhusu kifo tata cha mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’, yupo kwenye mazingira mazuri kueleza kilichotokea.

KWA NINI ANA USHAHIDI WOTE?
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mgaza Pembe ‘M2 The P’, ndiye mwenye ushahidi wote kwani aliambatana na Ngwea kila sehemu waliyotembelea mpaka nukta ya mwisho nchini Afrika Kusini.
M2 The P, alipatwa na matatizo sawa na marehemu Ngwea, isipokuwa mwenzake ilifikia hatua mbaya na kupoteza maisha huku yeye akibaki mahututi kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya St. Helen Joseph, jijini Johannesburg nchini humo.
Jambo la faraja ni kwamba, M2 The P yupo vizuri kwa sasa, atakaporuhusiwa kutoka, atajibu maswali mengi tata ambayo yamejitokeza tangu Ngwea alipofariki dunia Juni 28, mwaka huu, nchini humo  alipokwenda kwenye shughuli zake.

JAWABU LA SUMU 
Moja ya mambo yanayozungumzwa pembeni ni kwamba kuna uwezekano mkubwa marehemu Ngwea na M2 The P  waliwekewa sumu kwenye chakula au kupuliziwa ‘laivu’ kisha kutokea yaliyotokea, lengo likiwa kuwadhulumu mzigo wa fedha nyingi waliokuwa nao, hivyo kupona kwa mmoja huyo ni matakwa ya Mungu ili awe shahidi namba moja wa kifo cha Ngwea.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu jamani, M2 The P anaendelea vizuri sana, kwa sasa anazungumza. Naamini yeye amepona kwa ajili ya kufichua kilichofichika nyuma ya kifo cha mwenzake.
“Kama kweli walilishwa sumu kwenye chakula au walipuliziwa au lolote lile lingine, M2 The P anajua kila kitu kwani walikuwa wote kwa siku nzima mpaka wanarudi nyumbani alfajiri kwa safari ya kurudi Bongo.

“Awali tuliposikia M2 The P naye amefariki dunia sisi Wabongo wa huku tuliumia sana, tukasema sasa nani atafichua kilichotokea? Lakini Mungu mkubwa,” alisema Tony, Mbongo anayeishi Sauzi akifanya biashara halali.

HOFU YA KUUAWA M2 THE P
Baadhi ya watu waliishauri Serikali ya Tanzania kufanya kila liwezekanalo, M2 The P alirudi Bongo wakidai kama kweli wawili hao walilishwa sumu kwa namna yoyote ile, wahusika watafanya juu chini kuuondoa uhai wake ili kupoteza ushahidi.
Walisema kama ni sumu, wahusika watakuwa bado wapo ndani ya nchi hiyo na kwa vile M2 The P hana ndugu wa damu kule, si rahisi kulindwa kwa kiwango cha kutambua nani mbaya kwake.

MADAI YA UNGA KWA M2 THE P
Kumekuwa na madai kwamba, Ngwea alifariki dunia kwa ‘kujiovadozi unga’ lakini kama kweli msanii huyo alikuwa akitumia ‘mambo’, madai hayo yanapingana na ukweli kuhusu M2 The P kwamba si mtumiaji wa unga.
Kwa maana hiyo kama M2 The P si mtumia unga kwa nini na yeye alikumbwa na dhahama ileile iliyomkumba mwenzake? Kuna zaidi ya kitu hapo.
Juzi, Uwazi liliwatafuta baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva waliowahi kufanya kazi karibu na M2 The P na kuwauliza kama wanajua chochote kuhusu madai ya msanii huyo kubwia unga kama Ngwea, wote walikanusha.
“Jamaa (M2 The P) hatumii unga, we si unaona hata afya yake? Mtu anayetumia unga anajulikana hata kwa macho kaka,” alisema Mbongo Fleva mmoja mwenye jina kubwa Bongo akitokea upande wa Temeke.
Ndugu mmoja wa karibu na msanii huyo alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai hayo, alisema aliwahi kusikia tetesi hizo mwaka jana, alipofanya uchunguzi alishindwa kupata ukweli huku mtuhumiwa mwenyewe akikataa katakata kubwia madawa ya kulevya.

DALILI  ZA MBWIA UNGA
Kwa mujibu wa kitaalam, binadamu anayetumia unga hupoteza nguvu na uwezo wa kufanya mambo aliyokuwa akimudu kuyafanya awali.
Akizungumza na Uwazi juzi, daktari wa zahanati moja iliyopo Kimara, Dar es Salaam (jina tunalo)  alitoa mfano wa kitaalam kwamba, mcheza mpira anayemudu kukaa uwanjani kwa dakika 90 anapotumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya hupoteza uwezo huo na pengine kumudu kuwepo kwa dakika 45 tu.
Alisema unga una tabia ya kummaliza nguvu mtumiaji, hasa asiye na uwezo wa kupata lishe nzuri hivyo kupoteza uwezo mkubwa wa awali, jambo linaloweza kuwafanya wengine kuona mabadiliko hayo ya wazi.
“Kuna mchezaji wa timu moja kubwa nchini, awali alikuwa akisifika kwa kucheza mpira vizuri, tena kwa muda wote, alipoanza kutumia unga uwezo wake uwanjani ulishuka kabisa na ikafika hatua akawa hapangwi hadi kiongozi mmoja wa timu alipombaini,” alisema dokta huyo.

M2 THE P ALICHEZA MPIRA KWA DAKIKA 90
Julai 7, 2012 kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini linalofanyika Uwanja wa Taifa, Dar kila mwaka (hata mwaka huu lipo), M2 The P alichezea Timu ya Bongo Fleva inayowashirikisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Msanii huyo alimudu kucheza mpira kwa dakika zote 90, hali inayoweza kuondoa wasiwasi kwamba ni mtumiaji wa unga kama inavyodaiwa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...