Monday, January 06, 2014

RAIS WA ZIMBABWE ROBERT MUGABE AZIRAI GHAFLA...!!!

mu 77055

Mtu kutoka ndani ya chama tawala cha serikali ya Zimbabwe amesema kuwa kiongozi wa muda mrefu na rais wa taifa hilo la Afrika, Robert Mugabe amezirai ghafla.

Happyton Bonyongwe, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Zimbabwe alilipotiwa akisema kwamba ulinzi umeimarishwa katika ikulu ya Zimbabwe, siku moja baada ya hofu ya kuzirai kwa Mugabe na hali yake yake ya kiafya kuenea nchi nzima.

Baba Jukwa, ambaye ni mtoa taarifa ndania ya chama tawala cha Zanu-PF ambaye anatumia mtandao wa facebook ameanika rushwa na ufisadi katika serikali ya Mugabe vimekithiri huku taarifa ya kuanguka na kuzirai kwa Mugabe zikiwa zimezagaa nchi nzima.
Hata hivyo, aliongeza kuwa Rais Mugabe hali yake ya kiafya si nzuri lakini katibu wa Rais huyo ndugu George Charamba, alikanusha taarifa hizo kwamba Mugabe ni mgonjwa.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

ANGALIA MAZISHI YA WAZIRI MGIMWA KATIKA PICHA

IMG 0035 1811f

IMG 0086 0993a

IMG 0095 4d12c
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

ASKARI WAWILI MBARONI KWA KUTEKA MAGARI MBEYA...!!!


 
Askari mwenye cheo cha sajini katika  Gereza la Ruanda na polisi mwenye cheo cha konstebo  katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mbeya, wamekamatwa kwa tuhuma za kushirikiana na watu wengine watatu, kwa kuteka gari  na kupora  fedha na mali  katika eneo la Mlima wa Kawetere, Barabara ya Mbeya-Chunya, juzi jioni.
Inadaiwa kuwa katika tukio hilo, watuhumiwa walipora Sh3.5 milioni  na mabegi yaliyokuwa na  vitu mbalimbali.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kushiriki katika kupora mali ya mfanyabiashara Sheedhar Paupeleti (38) baada ya kuteka gari alilokuwa akisafiria akiwa na watu wengine wawili.
Habari zilisema katika tukio hilo, dereva wa gari hilo Ezekiah Matatira, alifungwa pingu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema majambazi hayo yalikamatwa baada ya polisi kwenda katika  eneo la tukio, kutokana na taarifa zilizotolewa na wananchi kwa njia ya simu.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0020 ed8be
DSC 0021 61136
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...