Sunday, July 10, 2016

JE, WAMJUA MNYAMA MWENYE WIVU KUPITA KIASI....??!

Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali, yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea.

Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere, anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke, mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii. Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz. Pia tu-follow instagram @jambotz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...