Thursday, October 17, 2013

REFA ALIYEPIGWA NA YANGA MWAKA JANA KUCHEZESHA PAMBANO LA WATANI JUMAPILI TAIFA

01_d16d6.jpg
Na Princess Asia, Dar es Salaam
REFA aliyewahi kupigwa na wachezaji wa Yanga SC Machi mwaka jana timu hiyo ikifungwa 3-1 na Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Israel Nkongo Mujuni ndiye atakayepuliza filimbi katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya watani wa jadi, Jumapili.
Nkongo alipigwa na wachezaji wa Yanga baada ya kumtoa kwa kadi nyekundu beki Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa tayari amempa kadi nyekundu kiungo Haruna Niyonzima pia.
Stefano Mwasyika aliyehamia Ruvu Shooting alimtupia ngumi ya 'kibondia' Nkongo na Nadir Haroub 'Canavaro' alionekana kuhusika katika vurugu hizo wote wakafungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mashabiki wa Yanga SC walifanya vurugu kubwa na kuvunja viti Uwanja wa Taifa siku hiyo.

Yamepita hayo na Nkongo amepewa tena mechi ya Yanga. Marefa wote wanne walioteuliwa kuchezesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Simba na Yanga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wanatambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
Mbali na Nkongo atakayepuliza filimbi, wengine ni Hamisi Chang'walu atakayeshika kibendera upande wa jukwaa kuu na Ferdinand Chacha atakayeshika kibendera upande wa pili, wakati mezani atakaa Orden Mbaga.

MUSEVENI ATAKA WAPINZANI WAMUOMBE RADHI

col-kizza-besigye_3dbc4.jpgyuweri_71085.jpg

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewataka viongozi wawili waandamizi wa upinzani nchini Uganda kuacha mapambao ya kisiasa wasiyoweza kushinda na badala yake wajiunge na chama tawala cha National Resistance Movement-NRM.
 Bwana Museveni alimshutumu mpinzani wake Kizza Besigye na meya wa Kampala, Erias Lukwago kwa kupinga program za maendeleo za serikali na kutangaza uongo. Alitaka aombwe msamaha na wapinzani hao wawili.
Lakini wote Besigye na Lukwago walipuuza wito wa Museveni wakiuita mchezo wa kisiasa wa kutaka kupata uungaji mkono wa chama tawala katika mji mkuu ambako wapiga kura mara nyingi hawakiungi mkono chama tawala.
Rais Museveni na chama chake tawala cha NRM wamekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Lakini Lukwago anasema matamshi ya karibuni ya Museveni ni matokeo ya kile anachosema kinaonekana ni mgawanyiko katika chama tawala.
Lukwago alisema maafisa wa utawala mara kwa mara wanakataa kufanya kazi na wapinzani kuhusu wasi wasi wa umma shutuma ambazo wawakilishi wa chama tawala wanazikanusha hazina ukweli. Wanaushutumu upinzani kwa kuzorotesha juhudi za serikali za kuendeleza sheria na kanuni na kuhakikisha amani na uthabiti nchini humo. Kitu ambacho Lukwago hakubaliani nacho. Chanzo: voaswahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...