Wednesday, May 22, 2013

"WASANII WANAOVAA VIMINI KWENYE FILAMU HUWA WANAJIUZA", MWAKIFAMBA

lulu7177
RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amesema wasanii wanaovaa mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini kwenye sinema wanajiuza.
Mwakifwamba aliyasema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa ameongozana na msanii Riyama Ally.
Kauli hiyo ya Mwakifwamba imekuja siku chache baada ya sakata la uvaaji vimini na udhalilishaji wanawake na wototo kwenye filamu kuzungumziwa bungeni, Dodoma.

“Hili suala nimeshalikemea kwa muda mrefu sana... naamini kama ni watu wa kuelewa watakuwa wameelewa na wale ambao wanaendelea na hayo mambo maana yake ujue wana mambo yao.“Siyo wote wanaoingia kwenye filamu ni wasanii wa kweli, wengine wanatumia tasnia hii kutafuta mabwana ndiyo maana wanavaa mavazi ya ajabu ili waonekane, jambo ambalo tunalikemea kila wakati
"Sikatai wakati mwingine kuna ‘scene’ zitahitaji uhusika fulani kama uchangudoa lakini utakuta msanii anatakiwa kuvaa uhusika wa ofisini, yeye anavaa vinguo vya hovyo, maana yake ni nini kama si kutafuta soko?” alisema Mwakifwamba na kuongeza:

“Imefika wakati wasanii wanatakiwa wabadilike kwani hali ilipofikia siyo pazuri. Bado msanii anaweza kuonekana ana kiwango kizuri bila kuvaa nguo zinazomdhalilisha na kumtafsiri vibaya mbele ya jamii.”Akasema: “Sasa nasema hivi, yeyote atakayekiuka utaratibu tuliokubaliana tutamchukulia hatua. Hatutamfumbia macho. Tunahitaji kuwa na tasnia yenye heshima.”RIYAMA SASA
Mkali wa kucheza na hisia, Riyama naye alitoa maoni yake kuhusu mavazi na mwenendo mzima wa filamu za Kibongo ambapo kwa upande wake alisema anaamini wanaofanya hivyo wanatafuta kuwa mastaa kwa njia ya mkato.
“Tatizo ni ulimbukeni wa kuiga wasanii wa nje. Wasanii tunakiwa kujitambua na kufahamu na kulinda utamaduni wetu. Wasanii wengi hawajui thamani zao, jamani ustaa siyo kukaa uchi.“Tujue kuwa kwenye filamu siyo sehemu ya kutafutia mabwana. Kuonesha urembo wetu wa nje na wa ndani kwenye hadhara siyo kitu kizuri kwa utamaduni wetu... hao wanaofanya hivyo wanasababisha wasanii wote tuonekane machangudoa,” alisema Riyama.

MASHABIKI NCHINI KENYA WAMZOMEA MR NICE HUKU WAKIMUITA MAC MUGA, HIVI NDIVYO ILIVYOKUA


Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa Iclub, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.


inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakua kama alivyotarajia. pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale, lakini Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidaikuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.

inasemekana mashabiki walipata kichekesho kipya pale ambapo Mr Nice aliponyanyuka na kusema " Hamnilipi mimi nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi" baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo  wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka

PAPA FRANCIS AKIRI KUPITIWA NA USINGIZI WAKATI IBADA IKIENDELEA..Angalia VIDEO

Papa Francis I wakati wa Ibada hiyo.
Papa Francis amekiri kusinzia wakati akisali mwishoni mwa siku ndefu, lakini alisema anafikiri Mungu 'ameelewa'.
 
Baba Mtakatifu huyo alikuwa amesimama mbele ya watu 200,000 waliokusanyika pamoja kwenye Viwanja vya Mtakatifu Petro pale alipotoa maoni ambayo hayakupangiliwa kuanzia kutoka kumbukumbu za bibi yake, uamuzi wake wa kuwa Padri na rushwa katika siasa.
Akisababisha vicheko kutoka kwa umati huo, alifafanua
jinsi anavyosali kila siku mbele ya madhabahu kabla ya kwenda kulala.
"Wakati mwingine nalala, kazi hiyo ngumu ya siku hukufanya ujikute umelala, lakini Mungu anaelewa," alisema.
Akiwataka Wakatoliki kuongeza juhudi kusaidia mafukara na wenye mahitaji katika jamii alisendelea: "Kama tukijitoa, tutakuta umasikini.
Leo, inaniuma kuzungumzia, kukutana na mtu asiye na makazi ambaye amekufa kutokana na baridi, sio habari.
"Leo, habari ni kashfa, hiyo ndio habari, lakini hao watoto wengi ambao hawana chakula - hiyo sio habari.
"Hili ni kaburi. Hatuweza kubweteka kirahisi tu wakati mambo yakiwa namna hii."
Miongoni mwa umati huo, ambapo wengi wao tayari wanajihusisha na kazi za kujitolea, walimkatiza mara kwa mara kwa makofi.
source zero99

AZAM MARINE WALETA MELI MPYA KALI ILE MBAYA, INAITWA KILIMANJARO IV

 Muonekano wa Kilimanjaro 4
 
KAMPUNI ya Azam Marine, inaleta boti mpya ya Kilimanjaro 4, ambayo inatarajiwa kuwasili nchini nchini, kuanzia mwishoni wa mwezi huu, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 700 na kutumia muda wa dakika 70 kwa safari moja ya kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Hii ni boti mpya kabisa katika muendelezo wa boti za Kilimanjaro, ambayo itakidhi mahitaji ya wasafiri wa eneo hili kwa kuwa inabeba sifa zote, ambazo ni Usalama, Kasi zaidi na Unadhifu. Kaa tayari kwa mzigo mpya kutoka Azam Marine.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Simba, Yanga kikaangoni Kagame

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye
Mabingwa watetezi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga wataanza kutetea taji lao dhidi ya Express ya Uganda katika mechi ya kundi C Juni 20 kwenye Uwanja wa Elfasher saa nane mchana wakati Simba iliyopangwa kundi A la 'kifo' itashuka dimbani siku inayofuata kuivaa El Mereikh.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo yatakayoanza Juni 18 hadi Julai 2 mwaka huu iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), timu nyingine zinazounda kundi C pamoja na Yanga ni Vital'O ya Burundi na Ports ya Djibouti wakati kundia la kundi A la Simba linahusisha pia timu za APR ya Rwanda na Elman ya Somalia.

Ratiba hiyo inaonyesha kuwa kundi B limezoa timu wenyeji zote tatu za Al Hilal, Al Nasri na Al Ahly Shandy pamoja na Tusker ya Kenya na Super Falcon kutoka Zanzibar.

Yanga ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara watashuka tena dimbani Juni 22 mwaka huu kuikabili Ports na watakamilisha mechi za hatua ya makundi Juni 25 kwa kuvaana na Vital'O.

SIMBA YAMPANDISHA NGASSA MAHAKAMANI, HIKI NDO SIMBA WALICHOKISEMA

Mrisho Ngassa akikabidhiwa jezi bada ya kujiunga na Yanga.
UONGOZI wa Simba umechukua uamuzi wa kumpandisha kizimbani kiungo mshambuliaji, Mrisho Ngassa kutokana na uamuzi wake wa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga.

Ngassa aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo kutoka Azam FC, amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga lakini Simba wamesema walishasaini naye mkataba wa mwaka mmoja.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, Msimbazi wameamua kufanya mambo yao kimya na wameamua kutumia mahakama ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
“Hakika sasa tumeona suala hili si la kufanya kama filamu, maana wenzetu (Yanga) pamoja na Ngassa wameamua kutufanyia uhuni. Wachezaji wanataka kufanya Simba ni kama sehemu ya kuchota fedha na kuondoka.
“Kitu kibaya zaidi tumegundua system (mfumo) ya soka imekuwa ikiwalinda sana kutokana na ushabiki mkubwa uliopo katika kamati zilizo chini ya TFF. Sasa sisi tumeona bora kuchukua hatua zaidi,” kilieleza chanzo cha uhakika.

UWOYA, JOHARI KUZURU SAUZI....!!!

Irene Uwoya.
MASTAA wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya na Blandina Chagula ‘Johari’ wametimkia nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kwenda kurekodi filamu. Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni kwa njia ya simu akiwa nchini humo, Uwoya alisema wamekwenda nchini humo kurekodi sinema ambayo Watanzania wataitambua ikikamilika. Pia wataunganisha na ziara ndefu katika nchi mbalimbali barani Afrika zikiwemo Namibia, Ghana, Lesotho na kwingineko kujifunza soko la filamu.
 
Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tupo huku na Johari lakini tutakuwa na ziara ndefu sana ya nchi mbalimbali za Afrika kwa ajili ya kulisogeza soko letu la filamu na kujifunza jinsi wenzetu wanavyofanya katika filamu zao,” alisema Uwoya.

WASTARA RUKSA....... KUOLEWA

Wastara Juma.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo, zinasema kwamba Wastara amemaliza salama eda yake baada ya kufiwa na mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari, mwaka huu.
Staa huyo bado yupo Muscat, Oman alikoitwa na ndugu zake kwa ajili ya kukaa eda hiyo na kupumzika baada ya kupata masaibu ya kuondokewa na mumewe kipenzi.
KAMA MWARABU
Chanzo kinaeleza kuwa uamuzi wa Wastara kwenda kukaa eda Uarabuni ni mzuri kwa sababu kwa sasa yupo vizuri kiafya na mawazo ya kuondokewa na mwenzake yamepungua.
“Ni kweli kifo hakizoeleki lakini Wastara amejitahidi sana kutuliza kichwa chake. Ndugu zake wamemsaidia sana, wamekuwa naye katika kipindi hiki kwa upendo wa hali ya juu.


“Yaani ukimuona jinsi alivyopendeza utashangaa, ni kama Mwarabu kabisa. Mungu mkubwa sana jamani, kila mtu anafurahishwa na jambo hilo. Mungu ataendelea kumsimamia,” kilipasha chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake gazetini.


Wastara akiwa Uarabuni.
KUTUA BONGO

KAKA, DADA WANASWA WAKIDUU COCO BEACH, MCHEZO MZIMA ULIKUA HIVI!

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya Firauni. Usemi huu unakamilishwa na tukio la kunaswa kwa vijana wawili wenye undugu wa damu wakifanya mapenzi ‘wakiduu’ kando ya Ufukwe wa Bahari ya Hindi!
Vijana wawili wenye undugu wa damu baada ya kunaswa wakifanya mapenzi.
Imefahamika kwamba vijana  hao, kaka na dada (majina tunayo)  wamenaswa ‘wakiduu’ katika mapango yaliyopo kando ya Ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
TUKIO ZIMA
Tukio zima lilitokea mchana kweupe wa saa 9 na kudhihirisha habari za mara kwa mara zinazoeleza kwamba Ufukwe wa Coco umekuwa ukitumika kwa ufuska usiku na mchana.
Risasi Mchanganyiko lilinasa tukio hilo kwa kutumia mitambo maaalum iliyoelekezwa kando ya bahari.
Wawili hao walinaswa tangu walipokuwa wakiingia katika ufukwe huo na kuwafuatilia nyendo zao, hatua kwa hatua.
...Dada akiwa kaduwaa baada ya kukutwa akivinjali na kaka'ake.
DEMU ALIKUWA AKIZINGUA
Haikufahamika mara moja kama wawili hao walikuwa na makubaliano ya kwenda kuduu katika ufukwe huo au la, lakini kwa mbali ilionekana kama vile dada mtu alikuwa akizingua kwenda kutenda dhambi hiyo.
Picha za video zilizonaswa, zinamuonesha dada huyo akionekana kutoa upinzani pale alipokuwa akishikwashikwa na kaka yake.
Alionekana kama vile hakuwa tayari kwa mchezo huo.
Hata hivyo, kaka mtu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23-26 alikuwa akilazimisha kitu fulani ambacho kilionekana dhahiri kupitia kamera zetu.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 22.05.2013

DSC 0061 cd132
DSC 0057 39d87
DSC 0059 b2f55

UJIO WA RAIS OBAMA NCHINI TANZANIA KUINEEMESHA SERIKALI...!!

Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai. 
 
Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
 
Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...