Friday, May 16, 2014

BIRTHDAY YA RAY, JOHARI AMPA SALAMU TATA..... ISOME HAPA....!!!

http://jambotz8.blogspot.com/
Leo ni birthday ya mwigizaji Vicenti Kigosi ray, Johari ampa salamu tata, isome hapa
Leo mwigizaji maarufu nchini Vicent kigosi - Ray anasherehehea siku yake ya kuzaliwa huku akipata salamu mbalimbali za pongezi toka kwa mastaa wenzie. Moja ya watu wa kwanza kwanza kumpa salamu hiyo ni swahiba na rafiki yake mkubwa, JB akifuatiwa Johari ambaye salamu yake inadaiwa na wachunguzi wa mambo kuwa ni kwa namna flani inamponda mpenzi wa sasa wa Ray, Chuchu Hans, kutokana na maneno yaliyotumika ya salamu hiyo ambayo Johari anadaiwa kuwahi kuyatumia kumponda Chuchu siku za nyuma.

JB ameandika
''Happy birth day mdogo wangu Ray. Mungu akupe haja ya moyo wako.''

Na huku Johari akiandika 
''Happy birthday director wa RJ na swaiba wangu Mungu akuongoze akupe maisha marefu na akuepushe na ‘’mabarazuri’’
Jambo Tz inakupongeza sana Ray kwa kutimiza miaka kadhaa siku ya leo na  Mungu akupe maisha marefu zaidi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WASSIRA AWATISHA UKAWA


Stephen Wassira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wassira amewatisha wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba wasiporejea bungeni, kanuni zitabadilishwa na Bunge litaendelea.
Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema: “Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema Wassira. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ATOA KAULI YA KUWABAGUA WANZANZIBAR BUNGENI...!!!

weremapx_89c87.jpg
Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema 'amelikoroga na kulinywa mwenyewe', baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka.
Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni na kuwaangukia akiwaomba radhi waliokerwa na kauli yake na pia kuliomba radhi Bunge, Spika wake, Anne Makinda na wananchi.

Kuondoka kwa wabunge hao kulitokana na mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ole (CUF), Rajabu Mbarouk Mohamed kutokana na majibu Jaji Werema kwa mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habibu Mnyaa aliyekuwa ameomba ufafanuzi wakati Bunge lilipokaa kama kamati ya kupitisha vifungu vya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2014/15. Mnyaa alisema Wizara ya Katiba na Sheria ni muhimu lakini imekuwa ndiyo ya kwanza kuvunja sheria na haki za binadamu na akataka ufafanuzi.

Hata hivyo, aliposimama kujibu swali hilo, Jaji Werema alimwambia Mnyaa kuwa mambo mengine akaulize Zanzibar na siyo katika Bunge la Jamhuri kwa kuwa si kila kitu kitaulizwa ndani ya Bunge hilo. "Alichokizungumza Mnyaa ni sahihi lakini hapa si mahali pake, namshauri kuwa akaulize huko Zanzibar kwenye vikao vyao hapa sisi hatuna majibu," alisema Werema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATALII TOKA UINGEREZA WATOROKA MOMBASA


Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya. Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba zikihofia usalama wao.

Gazeti la The Telegraph linasema kuwa takriban watalii 500 kutoka Uingereza wataathirika na kauli hiyo. Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya. Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.

Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa. Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.
Al Shabab
Al-Shabab imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi punde kundi hilo likisisitiza kuwa linalipiza kisasi vitendo vya majeshi ya Kenya nchini Somalia. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 16, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...