Monday, November 10, 2014

UTATA TENA: MISS TANZANIA MPYA SI RAIA WA TANZANIA...??!

Baada ya taji la Miss Tanzania kuvishwa kwa mshindi wa pili, utata mwingine umeibuka baada ya mrithi huyo, Lilian Kamazima kudaiwa kuwa si raia.

Jana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa Lilian siyo raia wa Tanzania na kwamba anatokea Rwanda.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim ‘Uncle’ Lundenga alisema tuhuma hizo kuhusu Lilian siyo kweli. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE 'AMWAGA SUMU' NYUMBANI KWA SAMUEL SITTA...!!!


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwasili kwenye Uwanja wa Extended mjini Urambo, Tabora alikohutubia mkutano wa hadhara juzi. 


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa Urambo Mashariki na kumshutumu Mbunge wa jimbo hilo, Samuel Sitta kwa kuchakachua maoni ya wananchi katika mchakato wa Katiba Mpya.

Katika mkutano huo ulifanyika katika Uwanja wa Extended mjini hapa takriban mita 100 kutoka nyumbani kwa Sitta aliyeongoza Bunge la Katiba, Mbowe alisema historia ya nchi hii itamhukumu mbunge huyo kwa maovu hayo.

Alisema kutokana na uovu huo wa Sitta ambaye amekuwa akiisifia Katiba Inayopendekezwa kuwa itakuwa nzuri Afrika Mashariki na Kati, vyama vya upinzani vitaendelea kuidai katiba ya wananchi hata kwa miaka 100 ijayo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

IKULU: "TUMEFEDHEHESHWA KWA KITENDO CHA JAJI WARIOBA KUSHAMBLIWA"


Balozi Ombeni Sefue


Serikali inapitia upya ulinzi wa viongozi wastaafu ili kuepuka fedheha iliyotokana na vurugu alizofanyiwa Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba hivi karibuni.

Mpango huo umeelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mwishoni mwa wiki, akisema Serikali imekerwa na kufedheheshwa kutokana na tukio hilo lililotokea wakati wa mdahalo wa Katiba Inayopendekezwa katika Hoteli ya Blue Pearl, Dar es Salaam Novemba 2, mwaka huu.

“Kimsingi tutakachokifanya ni kupitia upya mpango wa ulinzi wa viongozi wote waliostaafu, japokuwa huwa tunafanya hivyo mara kwa mara, lakini kwa hili la Mzee Warioba tunaliangalia kwa umakini wake.

“Tumekerwa sana na tukio lile, halikutufurahisha hata kidogo kama Serikali kwa kuwa limemvunjia heshima Mzee Warioba, yule ni mzee wetu, anahitaji heshima, kwanza heshima yake na ulinzi.”

Kauli hiyo ya Sefue imekuja wakati mdahalo huo uliovunjika baada ya Mzee Warioba kushambuliwa, ukiwa umetangazwa kufanyika upya Jumapili Novemba 16, mwaka huu katika hoteli hiyohiyo.

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole alithibitisha jana kuandaliwa kwa mdahalo huo kuanzia saa 9.00 alasiri siku hiyo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 10, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

'KURA YA MAONI MWANZO WA KUDAI KATIBA MPYA'


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo - Bisimba akizungumza na waandishi wa Gazeti la Mwananchi katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni Dar es Salaam.

Wakati Serikali ikihaha kuhakikisha inaandika historia mpya kwa kupitisha Katiba Inayopendekezwa Aprili 30, mwakani, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo – Bisimba amesema siku hiyo itakuwa mwanzo wa Watanzania kudai Katiba Mpya.

Dk Kijo – Bisimba, mmoja wa wanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini, amesema katika mazingira ambayo mchakato wa Katiba una dosari nyingi, ilikuwa ni busara kuusimamisha kwanza ili kujitathmini kabla ya kuendelea na Kura ya Maoni.

Mhitimu huyo wa shahada ya uzamivu ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Warwick, Uingereza, alisema hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika wiki iliyopita.

“Katiba hata ikiwa nzuri kiasi gani, kama haitokani na wananchi, haiwezi kukubalika,” alisema Dk Kijo – Bisimba akisisitiza hoja yake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MLIPUKO WATIKISA SHULE NIGERIA

Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati watoto wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo hakuna taarifa kamili kuhusu idadi ya majeruhi kufikia sasa.
Mlipuko huo ulitokea katika shule ya mafunzo ya sayansi ya vijana mjini humo.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram huenda ndilo limefanya shambulizi hilo, ila taarifa bado hazijathibitisha hilo.
Kundi hiulo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5 likitaka kuunda dola ya kiisilamu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

RAIS OBAMA AIZUNGUMZIA IRAQ

Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Obama amesema awamu ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuandaa serikali ya pamoja na yenye kuaminika nchini Iraq. Kitu ambacho amesema kimefanyika, na kuongeza kwamba muungano huo wa kijeshi unaopambana dhidi ya kundi hilo la wapiganaji unajiandaa kwa mashambulizi.
Tulichojua ni kwamba awamu ya kwanza iulikuwa ni kupata serikali ya umoja wa Kitaifa na ya uhakika Iraq. Na tumefanya hicho. ''..Na sasa tulichofanya ni zaidi ya kulimaliza nguvu kundi hilo la ISIL.
Kwa sasa tupo katika nafasi ya kuanza tena mashambulio kama ya awali. Mashambulizi ya anga yaliyofanywa yalifanikiwa katika kushusha uwezo wa kundi hilo la ISIL na kupunguza nguvu hatua waliyopiga.
Sasa tunachohitaji ni jeshi la ardhini, Jeshi la ardhini la Iraq, litakaloweza kuwarudisha nyuma..'' Nchini Iraq kwenyewe maafisa wanasema jeshi limekuwa likipiga hatua katika jihada za kuwaondoa wapiganaji hao wa kiislamu katika mji wa Baiji. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...